Shujaa wamewasili mjini Sydney baada yakuwapa Blitz Bokke wa Afrika Kusini kichapo ambacho hawaku tarajia mjini Hamilton New Zealand.
Nahodha wa Shujaa Andrew Amonde alipo zungumza na SBS Swahili alisema kwamba: "Tuko katika kundi gumu lakini tumejiandaa ipaswavyo, na wachezaji wetu wako tayari kushindana na timu yoyote katika michuano ya Sydney 7s. Tuna waomba mashabiki waje kwa wingi, sababu support yao ni muhimu sana kwetu."
Bila shaka Shujaa wamejipata katika kundi gumu sana ambalo lina jumuisha, Wales, Fiji na New Zealand. Mechi ya kwanza ya Shujaa itakuwa dhidi ya Fiji tarehe 1 Februari 2020, saa nane na dakika tisa, katika uwanja wa Bankwest Stadium, mjini Parramatta NSW.
SBS Swahili itakupa matokeo yote ya mechi za shujaa kupitia mitandao yetu yakijamii na katika tovuti hii.