Anthony Albanese amedai ushindi katika uchaguzi wa shirikisho wa 2025, wakati chama cha Labor kina jiandaa kuongoza kwa muhula wa pili kikiwa chama cha wengi.
Albanese ali waeleza wanachama mjini Sydney kuwa kuhudumu kama waziri mkuu, ilikuwa heshima kubwa ya maisha yake.
"Ni kwa hisia ya kina ya unyenyekevu na hisia ya kina ya uwajibikaji kuwa kitu cha kwanza ninacho fanya usiku wa leo nikusema 'asante' kwa watu wa Australia kwa fursa yaku endelea kuhudumu nchi bora duniani" alisema.
"Leo, watu wa Australia wame pigia kura maadili ya Australia: haki, matumaini na fursa kwa kila mtu.
"Wa Australia wame piga kura kwa siku za usoni zinazo ambatana na maadili haya, siku za usoni zinazo jengwa kwa kila kitu kinacho tuleta pamoja."
Labor itaongoza pekee yake ikiwa na ongezeko ya wabunge baada ya serikali kupata matokeo mazuri katika majimbo kadhaa.
Miongoni mwa faida kwa Labor ilikuwa kiti cha Dickson ambacho kilicho kuwa eneo bunge la Kiongozi wa Upinzani Peter Dutton jimboni Queensland.
Dutton alipoteza kiti chake kwa mgomea wa Labor Ali France, matokeo yaliyo mpa nafasi yaki pekee katika historia ya Australia yakuwa kiongozi wa kwanza wa upinzani, ambaye amepoteza kiti chake katika uchaguzi wa shirikisho.

Australian Liberal Party leader Peter Dutton, third left, stands with his family as he makes his concession speech following the general election in Brisbane. Source: AP / Pat Hoelscher/AP
"Hatukufanya vizuri yakutosha katika kampeni hii, hiyo ni wazi usiku wa leo," alisema.
"Nimetaka daima katika maisha ya umma vitu bora kwa nchi yetu na kila mu Australia.
"Ni tukio laki historia kwa chama cha Labor, na tuna tambua hilo."
Miongoni mwa sera zilizo tangazwa na Albanese kulikuwa kuwa ruhusu wanao nunua nyumba kwa mara ya kwanza kuingia katika soko la nyumba wakiwa na amana ya asilimia 5, wakati chama tawala kili ahidi kufanya matumizi ya $10 bilioni kujenga takriban nyumba mpya 100,000.
Ali ahidi pia uwekezaji wa $8.5 bilioni kwa huduma za ziada milioni 18 za madaktari za ruzuku, kila mwaka kama sehemu ya kuimarisha Medicare.
Chama cha Labor kime ahidi pia $2.3 bilioni kutoa ruzuku kwa betri za nyumbani zihifadhi umeme wa solar, wakati pia iki ahidi kuchukua hatua dhidi ya masoko kuongeza bei za bidhaa sana.