Australia kuwakatalia visa wahalifu wa unyanyasaji majumbani

Australia itakataa kutoa visa kwa watu wenye hatia ya ukatili.

Immigration Minister David Coleman.

Immigration Minister David Coleman. Source: SBS

Wageni wa Australia wanaweza kukataliwa kuingia au kufukuzwa nje ikiwa wamehukumiwa kwa unyanyasaji wa majumbani, chini ya maagizo ya serikali mpya ya shirikisho.

Uamuzi wa Waziri wa Uhamiaji David Coleman ulianza kutumika Alhamisi, kuzuia mtu yeyote ambaye amefanya vurugu dhidi ya wanawake au watoto hapa nchini.

"Ikiwa umehukumiwa na kosa la uhalifu dhidi ya wanawake au watoto, hamkubaliki," Mr Coleman alisema.

"Popote ambapo kosa limetokea, hukumu yoyote, Australia haitakuwa na uvumilivu kwa wahalifu wa majumbani."

Alisema mwelekeo huo utatumika sio tu kwa watunga maamuzi ndani ya Idara ya Mambo ya Ndani, lakini pia kwa Mahakama ya Rufaa ya Utawala. 

"Kumekuwa na idadi kadhaa ambapo waamuzi katika serikali wamekataa visa kwa mtu aliyekuwa na hatia ya unyanyasaji wa nyumbani.


Share
Published 4 March 2019 12:01am
By Frank Mtao
Presented by Frank Mtao


Share this with family and friends