Taarifa mpya kuhusu COVID-19: Australia yatazamia 'uchumi uliochanjwa' baada yakufunguliwa kutoka janga

Hii ni taarifa mpya kuhusu Coronavirus nchini Australia kwa 24 Oktoba 2021.

Kiongozi wa Victoria Daniel Andrews, amesema anataka idadi ya watu 80,000 wahudhurie mechi ya kriketi ya Boxing Day Test.

Kiongozi wa Victoria Daniel Andrews, amesema anataka idadi ya watu 80,000 wahudhurie mechi ya kriketi ya Boxing Day Test katika uwanja wa MCG, Melbourne. Source: AAP

  • Serikali ya shirikisho yatoa mradi mpya wa chanjo kwa wa Australia wa Kwanza.
  • Queensland kuweka zahanati za chanjo katika fukwe
  • Victoria yatoa mpango wake wakufungua jimbo kwa kiwango cha 90% ya chanjo

Victoria

Victoria inaratajiwa kufikisha lengo ya kiwango cha 80% ya chanjo wikendi ijayo. Uhuru wakusafiri jimboni humo utaanza Ijumaa 29 Oktoba.

Kiongozi wa jimbo hilo Daniel Andrews amesema kuwa Victoria inatarajia kutoa kiwango cha 90% ya chanjo, kwa umma wenye miaka 12 na zaidi kufikia 24 Novemba.

Bw Andrews aliongezea kuwa, "Hii inamaana kwamba, hapatakuwa vikomo popote, hapatakuwa maswali ya wingi popote."

Hata hivyo, masharti ya dozi mbili ya chanjo yata endelea kufuatiliwa.

"Uchumi wa chanjo hauendi popote," alisema kiongozi wa jimbo.

Jimbo hilo limerekodi kesi mpya 1,935 ndani ya jamii pamoja na vifo 11. 

Bonyeza hapa  leo.

New South Wales

New South Wales imerekodi kesi mpya 296 za maambukizi ndani ya jamii, pamoja na vifo vinne.

Jimbo hilo limetoa zaidi ya 84% ya chanjo kwa umma wenye zaidi ya miaka 16.

Serikali ya jimbo imezindua kampeni mpya kwa jina la 'Feel New South Wales' kukuza utalii baada ya jimbo hilo kufunguliwa tena.

Pata  kilicho karibu yako.

Queensland

Queensland haija rekodi kesi yoyote leo.

Serikali ya jimbo inashirikiana na shirika la Surf Lifesaving Queensland kuweka zahanati katika fukwe za jimbo hilo katika wikendi ijayo.

Hali ilivyokuwa nchini Australia katika masaa 24 yaliyo pita

  • ACT imerekodi kesi mpya 9 ndani ya jamii.
  • Serikali ya shirikisho imetoa kampeni mpya ya chanjo kwa jina la 'sambaza uhuru' pamoja na kampeni inayo lenga jamii yawa Australia wa kwanza kwa jina la 'sisi sote', kati ya wasiwasi kuhusu viwango vidogo vya chanjo miongoni mwa wa Australia wa kwanza.
  • 86% yawa Australia kwa sasa wamepokea dozi yao ya kwanza ya chanjo, wakati idadi hiyo inaendelea kusalia kuwa 60% kwa wa Australia wa kwanza.

Karantini, safari, zahanati za vipimo na malipo ya janga

Karantini na masharti yavipimo husimamiwa nakutekelezwa na serikali zamajimbo na wilaya:

ACT  na 
Kama unataka safiri ng'ambo, unaweza omba kibali mtandaoni.  kwa taarifa zaidi kuhusu masharti yakuondoka Australia. Kuna hatua za mpito kwa safari zakimataifa ambazo hutathminiwa mara kwa mara na serikali, nakuchapishwa kwenye tovuti ya .



Tazama rasilmali zilizo tafsiriwa za huduma yamawasiliano ya shirika la afya ya tamaduni nyingi ya NSW:


Zahanati za vipimo katika kila jimbo na wilaya:

 
 

Taarifa kuhusu malipo ya janga katika kila jimbo la wilaya:

 
 

Share
Published 24 October 2021 4:55pm
By SBS/ALC Content
Presented by Gode Migerano
Source: SBS


Share this with family and friends