Taarifa mpya kuhusu UVIKO-19: Makatazo yakubaki ndani katika Wilaya ya Kaskazini yaongezwa kwa muda wa siku saba

Hii ni taarifa mpya kuhusu Coronavirus nchini Australia kwa 16 Novemba 2021.

Kiongozi wa Wilaya ya Kaskazini Michael Gunner amewahamasisha wakaazi wa NT wafanye vipimo na wachanjwe

Ministro Chefe do Território do Norte, Michael Gunner fez um apelo para que comunidades indígenas se vacinem. Source: AAP Image/Aaron Bunch

  • Hatua yakufungiwa ndani kwa muda wa siku tatu katika eneo la Katherine katika Wilaya ya Kaskazini, imeongezwa kwa muda wa siku saba baada yakupatikana kwa kesi mpya tisa. Kesi zote katika wilaya ya kaskazini zinawahusu watu kutoka jamii yawa Aboriginal. Kiongozi wa Wilaya hiyo Michael Gunner ame hamasisha jamii zote zichanjwe.
  • Queensland imefungua tena mipaka yake kwa wasafiri kutoka NSW pamoja nakuanzisha mfumo wa karantini ya nyumbani.
  • Uchunguzi wa wiki tano kwa vifo vya coronavirus katika makazi ya huduna ya wazee ya St Basil's imeanza jimboni Victoria, ambako moja ya mlipuko mkubwa zaidi ndani ya makazi ya wazee unachunguzwa.
  • Huduma ya msaada yakitaifa kwa wanao hitaji msaada wakusoma nakuandika, imerekodi 46% ya ongezeko ya simu tangu Oktoba, kwa sababu ya taarifa za afya zinazo changanyisha, kuhusiana na chanjo ya UVIKO.
  • Bunge la Victoria lina jadili pendekezo la sheria za janga, wakati maandamano yana endelea kushuhudiwa.

TAKWIMU ZA UVIKO-19:

Victoria imerekodi kesi mpya 797 ndani ya jamii pamoja na vifo vinane. 
NSW imerekodi kesi mpya 212 ndani ya jamii pamoja na vifo viwili. 
ACT imerekodi kesi mpya 12 ndani ya jamii na, NT imerekodi kesi mpya 9.
New Zealand imerekodi idadi kubwa zaidi ya kesi zikiwa ni 222, tangu mwanzo wa janga pamoja na kifo kimoja.


Karantini, safari, zahanati za vipimo na malipo ya janga

Taarifa kuhusu UVIKO-19 na safari 





Tazama rasilimali zilizo tafsiriwa nakuchapishwa na Huduma Yamawasiliano na Afya ya Tamaduni nyingi ya NSW:



Zahanati za vipimo katika kila jimbo na wilaya:

 
 


Taarifa kuhusu malipo ya janga katika kila jimbo na wilaya:

 
 
 


Share
Published 16 November 2021 3:01pm
By SBS/ALC Content
Presented by Gode Migerano
Source: SBS


Share this with family and friends