- Victoria yaondoa vizuizi mapema kuliko ilivyo tarajiwa
- NSW yafikia 80% ya watu ambao wamepata chanjo mbili
- Mpangilio wa usafiri kati ya Australia na New Zealand kuanza tena wiki hii
- Serikali ya Australia yanunua 'Tiba' ya COVID-19
Victoria
Victoria yarekodi kesi mpya 1,838 za COVID-19 ndani ya jamii pamoja na vifo saba.
Kuna watu 777 ambao kwa sasa wako hospitalini, 151 wako katika kitengo cha huduma mahtuti pamoja na watu 94 ambao wanapumua kwa msaada wa mashine.
Kiongozi wa jimbo hilo Daniel Andrews alitangaza mapema kuliko ilivyo tarajiwa. Vizuizi vitaregezwa kuanzia usiku wa manane wa Alhamisi 21 Oktoba. “Vizuizi vikiondolewa, hapatakuwa vizuizi kwa watu kuondoka nyumbani, hapatakuwa amri yakubaki ndani," Kiongozi huyo alisema.
Asilimia 89 yawatu wa Victoria wenye umri wa miaka 16 na zaidi, wame pata dozi moja ya chanjo ya COVID, na asilimiia 65.5 yawatu wa Victoria wamepata chanjo kamili.
New South Wales
NSW imerekodi kesi mpya 301 za COVID-19 ndani ya jamii, pamoja na vifo 10.
Kiongozi wa jimbo hilo Dominic Perrottet alisema jana kuwa NSW imefikisha lengo la 80% la chanjo mbili, hali ambayo inamaanisha kuwa vita ondolewa.
Bw Perrottet ametangaza uwekezaji wa $130 milioni kwa afya ya akili.
"Sisi ni jimbo la kwanza Australia kuanza kutoa mafunzo kwa watu 275,000 kwa swala la kuzuia kujiua na huduma ya kwanza ya afya ya akili," Waziri wa Afya ya Akili Bronnie Taylor alisema.
Hali ilivyokuwa nchini Australia katika masaa 24 yaliyo pita
- Serikali ya shirikisho imenunua tiba elfu kumi na tano za Ronapreve.
- Usafiri bila karantini utaanza tena kati ya NSW na Vic na sehemu za NZ kuanzia usiku wa manane wa Jumanne 19 Oktoba.
- ACT imeripoti kesi mpya 33 za maambukizi ya COVID.
- Tasmania haija rekodi kesi yoyote mpya.
- Serikali ya Queensland haija weka tarehe yakufungua tena mipaka yake.
Karantini, safari, zahanati za vipimo na malipo ya janga
Karantini na masharti yavipimo husimamiwa nakutekelezwa na serikali zamajimbo na wilaya:
Kama unataka safiri ng'ambo, unaweza omba kibali mtandaoni. kwa taarifa zaidi kuhusu masharti yakuondoka Australia. Kuna hatua za mpito kwa safari zakimataifa ambazo hutathminiwa mara kwa mara na serikali, nakuchapishwa kwenye tovuti ya .
- Pata hapa habari na taarifa katika zaidi ya lugha 60
- Pata hapa miongozo inayo faa kwa jimbo au wilaya yako: , , , , , , .
- Pata hapa taarifa kuhusu .
Tazama rasilmali zilizo tafsiriwa za huduma yamawasiliano ya shirika la afya ya tamaduni nyingi ya NSW:
Zahanati za vipimo katika kila jimbo na wilaya:
Taarifa kuhusu malipo ya janga katika kila jimbo la wilaya: