1. Weka hela za akiba
Malipo ya asilimia 10 ya bei ya nyumba yanahitajika unapo nunua nyumba. Hata hivyo, wanunuaji wanaweza epuka malipo ya ziada kwa kampuni za dhamana zinazo kopesha hela zaku nunua nyumba iwapo wana weka asilimia 20 ya bei ya nyumba. Kama ume weka hela zakutosha, hatua inayo fuata ni ombi lako la mkopo kukubaliwa.
Image
2. Chunguza aina ya mikopo ya nyumba na hakikisha ombi lako la mkopo linakubaliwa.
Jua idadi ya hela unazohitaji kununua nyumba, kabla yaku amua aina ya mkopo unao hitaji, uliza watakao kupa mkopo huo wakupe maelezo kamili uyalinganishe na mikopo mingine ambayo iko sokoni.
Image
3. Kopa kulingana na mapato/uwezo wako.
Kuwa makini usikope zaidi ya uwezo wako. Haitakuwa vizuri kujipata katika hali ambayo unalazimishwa kuuza nyumba yako kwa sababu hauwezi timiza masharti yaku lipa mkopo wa nyumba.

Source: Getty Images
4. Wekeza hela kwa ripoti ya ukaguzi
Ukaguzi wa jengo huenda uka kugharimu ma mia ya dola ila, inaweza kuokolea maelfu ya dola kwaku epuka matatizo ukisha hamia ndani ya nyumba.

Source: Getty Images