Lengo la operesheni hiyo ilikuwa kuzungumza na mtu yeyote ambaye maafisa hao wanakutana naye kuhakikisha ana visa/kibali halali cha kuwa nchini.
Ila dakika chache kabla maafisa wa Idara ya Ulinzi wa Mipaka na Polisi Victoria wazungumze na waandishi wa habari, mbele ya kituo kikuu cha treni cha Mtaa wa Flinders mjini Melbourne, maelfu ya waandamanaji walijumuika mbele ya kituo hicho kuonesha hasira yao dhidi ya oparesheni hiyo.
Waandamanaji waliendelea kuongezeka katika eneo hilo na punde baadae walijumuika katikati ya barabara ambako magari na treni yalikabiliwa na kibarua chakuendelea na safari zao.

Waandamanaji waonesha hisia zao dhidi ya oparesheni ya idara ya ulinzi wa mipaka mjini Melbourne Source: Picha: ABC News
Taarifa hizo zilipo sambaa katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, Idara ya ulinzi wa mipaka na Polisi wa Victoria walitangaza kwamba oparesheni hiyo imefutwa.
Hii hapa video fupi iliyorekodiwa na mtangazaji wa Idhaa ya SBS Punjabi.
'Refugees are welcome, border forces not'A group of 'anti-racism' activists stage a protest outside Flinders Street station against Australian government's alleged 'anti-refugee' policies. Posted by SBS Punjabi on Thursday, August 27, 2015
Je ulishuhudia/ulishiriki katika maandamano hayo? wasiliana nasi/tuma maoni yako hapa: [email protected]