Afya nzuri maishani hupunguza uwezekano wa mshtuko wa moyo ila, ikitokea unastahili kumbuka dalili na uchukua hatua haraka.
Nini hutokea mtu anapo kumbwa kwa mshtuko wa moyo?

Source: Pixabay
Umeshauriwa umwone daktari wako, akufanyie unchuguzi wa afya ya moyo wako, nakutathmini athari yako, haswa kama una historia ya mishtuko ya moyo katika familia yako.
Je kuna aina gani za athari?
Shinikizo la damu
Ni wakati iko juu, moyo wako na mishipa inaweza lemewa. Ila inaweza tibiwa, kwa hiyo mwone daktari wako mara kwa mara ili achunguze shiniko la damu yaku.

Source: Anthony Devlin/PA Wire
Kiwango cha juu cha mafuta
Jaribu kuepuka matumizi ya mafuta mengi ndani ya chakula chako. ndani ya damu yako inaweza sababisha mshtuko wa moyo au kiharusi.
Chakula kibaya na kisukari
Vegetables and fruits Source: GettyImages/fcafotodigital
Shirika la Diabetes Australia nalo ya jinsi yaku kabiliana na kisukari chako, kusaidia kuepuka msthuko wa moyo.
Uhaba wa mazoezi ya mwili
Kutofanya mazoezi naku keti kwa muda mrefu, sivizuri kwa afya ya moyo wako. Wataalam wa afya wame pendekeza kufanya mazoezi kwa muda wa nusu saa kila siku. Mbinu nzuri yaku anza niku tembea!

Health is a must if you are into a road trip by motorhome Source: AAP
Kuvuta sigara
Una athari kubwa yakuwa na mshtuko wa moyo iwapo wewe ni mvuta sigara. ni moja ya mbinu nzuri yaku linda moyo wako. Unapo acha kuvuta sigara, athari ya ziada nayo hupungua.

Source: AAP
Kujitenga na jamii na huzuni nyingi
Watu ambao hawana uhusiano na jamii, familia au marafiki wanaweza kuwa na athari kubwa ya matatizo ya moyo. Huzuni yakupindukia nayo inaweza changia katika hali hiyo. Shirika la hupendekeza iwapo unakumbwa kwa huzuni yakupindukia kwa wiki mbili, zungumza na daktari wako, jamaa wako au mtu unaye mjua vizuri.
Hauwezi badili baadhi ya athari
Shirika la lime chapisha baadhi ya athari ambazo hatuwezi dhibiti, athari hizo ni kama: miaka, historia ya familia au ukoo wako. Kwa mfano, watu kutoka ukanda wa India wana athari kubwa yaku kabiliwa kwa mshtuko wa moyo kuliko watu wengine.
Baadhi ya dalili ni gani?
Kuhisi usumbufu na uchungu kifuani
Dalili za hatari hutofautiana toka mtu mmoja kwa mwingine, dalili ya kwanza yakutafuta ni uchungu kifuani. Unaweza hisi kubanwa katika maeneo yakifua.
“Iwapo ni shambulizi la papo hapo, maumivu kifuani yatakuwa mengi bila mwisho. Utayahisi upande wa kushoto wa kifua, ila inaweza kuwa katika maeneo ya katikati. Maumivu hayo yata gonga pia katika eneo la taya na katika mkono wa kushoto" hiyo ni kwa mujibu wa mtaalam wa moyo Rob Perel kutoka shirika la Heart of Australia.
Maumivu mikononi, shingoni na mgongoni
Maumivu yanaweza sambaa katika sehemu tofauti za sehemu ya juu ya mwili. Unaweza hisi mikono yako inakuwa mizito au kuto tumika ipasavyo.
Kuhisi unakosa pumzi
Unaweza hisi unakosa pumzi. Dalili zingine zinaweza jumuisha hisia yaku banwa kooni, kichefuchefu, kutokwa jasho baridi na kuhisi kizunguzungu.
Utafanya nini?

Source: AAP
Kitu cha kwanza chakufanya unapo kabiliwa kwa mshtuko wa moyo nikupigia simu nambari hii (000) na uombe gari la wagonjwa. “Wahudumu watakao jibu mwito wako, wata kupa dawa kwa jina la Aspirin watakapo wasili. Unastahili keti na upumzike, na uepuke kuweka shinikizo la ziada kwa moyo wako, hadi mtu mwingine atakapo kufanyia vipimo vya ziada naku kupa tiba." Hiyo ni kwa mujibu wa Rob Perel, mtaalam wa moyo kutoka shirika la Heart of Australia.