Mcheza tenisi nambari moja duniani kwa upande wa wanaume Novak Djokovic amepoteza ombi lake dhidi ya uamuzi wa serikali ya shirikisho kufutwai viza yake usiku wa kuamkia michuano ya wazi ya Australian.
Kesi hiyo ilisikilizwa Jumapili na benchi kamili ya majaji watatu wa Mahakama ya Shirikisho iliyojumuisha Jaji Mkuu James Allsop, Jaji Anthony Besanko na Jaji David O'Callaghan.
Jaji Mkuu Allsop alisema majaji hao watatu wameamua kwa kauli moja kuunga mkono kufutwa kwa viza ya Djokovic na serikali.
Jaji Mkuu Allsop alisema haikuwa "sehemu ya kazi ya mahakama" kuamua juu ya "sifa au hekima" ya uamuzi wa Waziri wa Uhamiaji Alex Hawke wa kufuta viza ya Djokovic.
Alisema mahakama "haikuwa na uwezo wa kutoa sababu leo" lakini hoja zaidi juu ya uamuzi wa mahakama itachapishwa "baadaye."
Mahakama pia iliamuru kwamba Djokovic alipe gharama za kisheria za serikali kwa kusikilizwa kwa kesi hiyo.
Uamuzi huo unamaanisha kuwa Djokovic, ambaye hajachanjwa dhidi ya COVID-19, hatashiriki michuano ya wazi ya Australian na anatarajiwa kufukuzwa kutoka Australia.
Mchezaji nambari 150 duniani Salvatore Caruso wa Italia sasa anajikuta akichukua nafasi ya Djokovic kileleni mwa droo hiyo ya michuano.
Djokovic alitoa taarifa Jumapili usiku akizungumzia matokeo ya kesi hiyo.
Alisema ingawa "amesikitishwa sana" na uamuzi huo, "atashirikiana na mamlaka husika kuhusiana na kuondoka kwake" kutoka Australia.
"Sasa nitachukua muda kupumzika na kupata nafuu, kabla ya kutoa maoni mengine zaidi ya haya," alisema. "Sina raha kwa mwelekeo wa wiki zilizopita ulivyokuwa kwangu na ninatumai kuwa sote sasa tunaweza kuzingatia mchezo na mashindano ninayopenda. "Ningependa kuwatakia wachezaji, viongozi wa mashindano, wafanyakazi, watu waliojitolea na mashabiki kila la heri kwa ajili ya mashindano."
Image
Waziri Hawke alikaribisha uamuzi wa Mahakama ya Shirikisho wa kuidhinisha kufutwa kwa viza ya Djokovic kwa "maslahi ya umma".
"Sera dhabiti za ulinzi wa mpaka wa Australia zimetuweka salama wakati wa janga hili, na kusababisha moja ya viwango vya chini vya vifo, urejeshaji madhubuti wa kiuchumi, na viwango vya juu zaidi vya chanjo ulimwenguni," alisema katika taarifa yake Jumapili. "Sera kali za ulinzi wa mpaka pia ni muhimu katika kulinda mshikamano wa kijamii wa Australia ambao unaendelea kuimarika licha ya janga hilo."
Image
Waziri Mkuu Scott Morrison aliunga mkono maoni haya katika taarifa yake Jumapili, akisema uamuzi ulifanywa kuweka "mipaka imara na kuwaweka Waaustralia salama."
"Kama nilivyosema Ijumaa, Waaustralia wamejitolea sana wakati wa janga hili, na wanatarajia matokeo ya kujitoa huko kulindwa," alisema. "Mipaka yenye nguvu ni msingi kwa njia ya maisha ya Australia kama ilivyo sheria. “Serikali yetu imekuwa ikielewa hili na imekuwa tayari kuchuku"a maamuzi na hatua zinazohitajika ili kulinda uadilifu wa mipaka yetu. "Sasa ni wakati wa kuendelea na Australian Open na kurejea kufurahia tenisi majira ya joto."