Soma kwa makini mkataba wako waku kodi nyumba
Mkataba waku kodi nyumba, ni hati yakisheria. Inajumuisha maswala kama, idadi ya hela unapashwa lipa na jinsi yaku lipa. Muda mkataba huo utakao dumu na aina ya upangaji, idadi ya dhamana inayo hitajika pamoja na masharti na sheria zingine. Hata hivyo, usitie saini karatasi ambayo hauelewi.

rental agreement form Source: Getty Images
Lipa dhamana yako
Dhamana yako ni malipo tofauti na kodi yako. Huwa inatumiwa kama kinga na mwenye nyumba iwapo hautimizi masharti ya mkataba wako wa upangaji. Kwa mfano mkoani Victoria, dhamana hiyo hulipwa kwa shirika hili ambako huwekwa hadi mwisho wa mkataba huo.

Scattered Australian Cash Source: Getty Images
Jaza ripoti kuhusu hali ya nyumba utakayo kodi
Unapo hamia ndani ya nyumba, jaza ripoti kuhusu hali ambayo nyumbo hiyo ilimo, jumuisha kila kitu ambacho kimo ndani ya nyumba hiyo kisha rejesha ripoti hiyo kwa wakala wa nyumba au mwenye nyumba katika siku saba. Wewe pamoja na mwenye nyumba mna stahili kuafikiana kuhusu ripoti hiyo kabla yaku weka saini.

Source: AAP/Tracey Nearmy
Hifadhi nakala ya kila kitu
Unashauriwa kuhifadhi nakala za maafikiano ya upangaji, ripoti ya mazingira ya nyumba, risiti ya malipo ya kodi na malipo ya dhamana, barua pepe pamoja na rekodi za maandishi.

Searching In File Cabinet Source: Getty Images
Fahamu haki na wajibu wako
Kwa mfano mkoani NSW, unahaki yaku pinga mwongezeko wa kodi au kuwasiliana na mwenyenyumba yako ambaye haja tekeleza wajibu wake, kwaku karabati nyumba yako, kwaku wasiliana na mahakama hii: .
Unaweza pata maelezo ya ziada kupitia video, maandishi kuhusu haki na wajibu wa wapangaji katika kila jimbo, mkoa na wilaya katika lugha mbali mbali.

Source: AAP/Julian Smith
Iwapo uko Victoria unaweza pata maelezo ya ziada katika tovuti hii: