Breaking

Rutto na Raila waingia rasmi katika ndoa ya kisiasa

Rais wa Kenya Dkt William Ruto na Kinara wa Upinzani nchini humo Raila Odiga, hatimae wame thibitisha uvumi kuhusu wawili hao kushirikiana katika uongozi wa taifa hilo.

Raila Odinga na William Rutto wakubaliana rasmi kuchangia uongozi.jpg
Kwa miezi kadhaa chama cha Raila Odinga, ODM kili sisitiza kuwa hakiko serikalini wala hakina ushirikiano wowote na serikali ya Dkt Rutto.

Rais Rutto na Raila Odinga wakiwa pamoja na washirika wao, katika hafla ya kutia saini makubaliano ya kuchangia uongozi.jpg
Madai hayo yali tolewa licha ya chama hicho kuwapa baraka viongozi wake wanne kuwa mawaziri katika serikali ya Kenya Kwanza.

Rais Rutto na Bw Odinga waliwasili katika ukumbi wa KICC, kutia saini makubaliano ya ushirikiano kati ya serikali ya Kenya Kwanza na chama cha upinzani cha ODM.

Raila Odinga na Rais Rutto na washirika wao, wa wasili katika ukumbi wa KICC, Nairobi, Kenya.jpg
Tukio hilo limepokewa kwa hisia mseto katika taifa hilo la Afrika Mashariki, wachambuzi na raia wakijumuika katika mitandao yakijamii kuchangia maoni yao.

Share
Published 7 March 2025 10:52pm
Updated 9 March 2025 3:53pm
By Gode Migerano
Presented by Gode Migerano
Source: SBS

Share this with family and friends