1. Mmoja kati yawa Australia wasita, ata athiriwa na kiharusi katika maisha yake.

2. Mtu mmoja kati yawatu watatu hufariki ndani ya kipindi cha mwaka mmoja baada yaku athiriwa na kiharusi.

Source: EPA
3. Kiharusi huwaua wanawake wengi kuliko saratani ya matiti na wanaume wengi zaidi kuliko saratani ya kibofu.

Source: Getty Images
4. Asilimia 20 yawatu ambao huathiriwa na kiharusi huwa chini ya umri wa miaka 55.

Source: Getty Images
5. Kuna uwezekano wanaume wanaweza athiriwa na kiharusi wakiwa na umri mdogo.

Source: AAP
6. Shinikizo ya damu ni moja ya athari kubwa zinazo julikana kusababisha kiharusi.
Shinikizo ya damu ni wakati shinikizo ya damu mwilini inazidi 140/90. Hali hii inajulikana kama hypertension au shinikizo ya damu. Kawaida shinikizo ya damu huwa 120/80.

Source: Press Association
7. Mtihani unaojulikana kwa jina: FAST ni mbinu rahisi yakutambua naku kumbuka ishara za kiharusi.
Mtihani wa FAST unajumuisha maswali rahisi kama: Sura- tazama sura ya mwathiriwa. Mdomo wake ume pengama? Mkono- mwathiriwa anaweza inua mikono yote mbili? Matamshi- je matamshi yake ya maneno yame badilika nakuwa pole pole zaidi? Wanakuelewa? Wakati- Wakati ni muhimu. Ukiona dalili hizi, pigia simu 000 mara moja.

Source: Courtesy of Stroke Foundation
8. Ishara za kiharusi zinaweza tokea moja baada ya nyingine au kwa mchanganyiko.

Source: Monty Rakusen/Getty Images
9. Baadhi ya tiba za kiharusi lazima zitolewe katika muda wa masaa 4.5 ya shambulizi la kiharusi kuanza, au wakati dalili za kiharusi zina jitokeza.

Source: AAP
10. Ni muhimu kupokea matibabu ya dharura
Kama unakabiliwa na kiharusi, matibabu ya dharura yanaweza okoa maisha yako na yanaweza punguza uwezekano wa uharibifu wakudumu wa ubongo. Daktari ndiye anaweza amua kama unakabiliwa na kiharusi ama ulikabiliwa na kiharusi.

Source: AAP