1. Ni lazima kila mtu ambaye yuko nchini ashiriki katika usiku wa sensa.
Si lazima uwe raia wa Australia, kujaza fomu ya sensa. Wanao tembelea familia zao nchini kutoka ng'ambo, wanafunzi wakimataifa, watu ambao wako nchini kwa viza 457 na hata watalii ambao wako nchini lazima wajaze fomu za sensa.

Source: Scott Barbour/getty
2. Taarifa unayo toa katika sensa, hutumiwa kupanga makazi, usafiri, elimu na hospitali.

General view of traffic on the Warringah freeway in Sydney, Wednesday, May 6, 2015. (AAP Image/Dan Himbrechts) NO ARCHIVING Source: AAP Image/Dan Himbrechts
3. Mwaka huu sensa itafanyiwa mtandaoni kwa mara ya kwanza.
Kuanzia Agosti mosi (1) utapokea barua ambayo ina namba na maelezo utakayo hitaji kutumia kujaza fomu yako ya sensa mtandaoni.

Source: Sharie Kennedy/Getty Images
4. Unaweza fanya sensa pia kwaku jaza karatasi ya sensa badala yaku ifanyia mtandaoni.
Kama unahitaji fomu hiyo, lazima uiombe kwaku piga simu kwa namba hii: 1300 214 531.

Blank UK Census form. Source: Getty Images
5. Unaweza omba msaada wa mkalimani, atakaye kusaidia kujaza fomu za sensa.

Source: Getty Images
6. Lazima ujibu kila swali katika fomu ya sensa isipokuwa swali kuhusu dini.
Swali la dini lime jibiwa kwa hiari tokea mwanzo wa historia ya Australia, uamuzi ulichukuliwa kwamba jibu kuhusu dini katika sensa lita tolewa kwa hiari. Ilhali ni lazima maswali mengine katika fomu ya sensa yajibiwe.

Source: Getty Images
7. Iwapo hauta jaza fomu za sensa, unaweza tozwa faini ya $180 kila siku hadi utakapo jaza fomu yako.

Source: AAP
8. Kama unaishi kandani au maeneo ya vijiji huenda ukatembelewa na afisa kutoka ofisi ya sensa ambaye ata kusaidia kujaza fomu yako.
Image
9. Jina na anwani utakalo andika katika fomu ya sensa haita changiwa na idara zingine za serikali.

Source: Public Domain/Pixabay
10. Kama uko ng'ambo usiku wa sensa, si lazima ujaze fomu ya sensa.

Source: Public Domain/Pixabay