1. Husika katika maisha yao
Fuatilia maslahi yao na panga ratiba yaku jumuika nao kila mara. Nimu himu kufanya vitu pamoja kama familia, kwa mfano kula pamoja kila siku.

Source: Getty Images
2. Sikiliza watoto wako
Wahamasishe wachangie matatizo yao nawe, bila kuwa na wasiwasi. Omba mchango wao katika uamuzi wa maswala ya familia, ili wahisi unathamini maoni yao.

Source: Getty Images
3. Kuwa mfano mzuri
Ni muhimu kuto puuza ushawishi wa tabia yako kwa watoto wako, haswa kwa maswala ya pombe, tumbaku au kutumia madawa vibaya.

Source: Getty Images
4. Kuwa mwaminifu nao
Hauta jua kila kitu kinacho husiana na mihadarati. Ukiwa mwaminifu na wazi kuhusu msimamo wako, itakuwa rahisi kwa watoto wako kuwa waaminifu nawe.

Source: Getty Images
5. Chagua wakati vizuri
Hakikisha unachagua wakati mzuri waku jadili mihadarati na watoto wako. Huenda ikawa wakati mna tazama runinga, au wanapo zungumza kuhusu mtu mwingine katika shule yao au katika kundi lao la marafiki.

Source: AAP
6. Kuwa mtulivu
Ni muhimu kuwa na mantiki na utulivu katika mjadala kuhusu mihadarati, pamoja nakuto kasirika haraka. Usiwakejeli wanao, kwa sababu hali hiyo inaweza fanya mijadala ya usoni kuhusu mihadarati kuwa migumu.Image
7. Epuka migogoro
Nivigumu kutatua tatizo wakati kuna mgogoro. Iwapo mgogoro unazuka, sitisha mazungumzo, hadi nyote mtakapo tulia.

Source: Pixabay/Public Domain
8. Endeleza mazungumzo
Unapo fanya mazungumzo ya kwanza kuhusu mihadarati, ni muhimu kuendeleza mjadala huo. Anza kuzungumza na watoto wako kuhusu mihadarati mapema, pia kuwa tayari kuzungumza na watoto wako kuhusu swala hili wakati wowote.

Source: Getty Images
9. Weka mipaka iliyo wazi
Jadili na kubaliana na watoto wako jinsi watafanya, watakapo jipata katika mazingira ambako kuna mihadarati. Kwa mfano, hakikisha wanajua utaenda kuwachukua iwapo wanahitaji msaada wakati wowote. Hata hivyo, hakikisha wanaelewa kuwa, ungependelea wasijiweke katika mazingira ambako huenda waka kabiliana na mihadarati.

Source: Getty Images