1. Si lazima usubiri masaa 24 kuwasilisha ripoti mtu anapo potea.

Source: Yui Yui Hoi/Getty Images
2. Ripoti ya mtu ambaye amepotea, inaweza tolewa katika kituo cha polisi kilicho karibu yako.
Ripoti zinazo wasilishwa kupitia simu zinakubaliwa tu katika mkoa wa Kusini Australia. Wasiliana na kituo cha polisi unako ishi kujadili mahitaji yako kama hauwezi fika katika kituo cha polisi kuwasilisha ripoti yako.

Source: Australian government
3. Toa maelezo kamili unapo wasiliana na polisi.
Itakuwa msaada mkubwa kwa polisi ukiwapa maelezo yakutosha kumtambua mtu ambaye amepotea. Maelezo hayo nikama; majina, maelezo ya mawasiliano ya marafiki wake, aina ya mapato yao ya Centrelink, maelezo ya pasipoti, mahitaji ya matibabu na maswala mengine yanayo kupa wasiwasi kuhusu ustawi wao.

Source: AAP
4. Unapo wasilisha ripoti ya mtu ambaye amepotea, huenda polisi wata chukua maelezo kamili mara moja.
Polisi wanaweza fanya uchunguzi nakuwasiliana nawe uwape maelezo ya ziada, iwapo mtu huyo hajapatikana katika muda mfupi.

Source: Rattlenoun CC BY SA 4.0
5 Hifadhi rekodi ya ripoti unayo wasilisha.
Huenda ikakufaidi kuhifadhi taarifa ifuatayo- namba ya uchunguzi wa tukio, kituo cha polisi na jina na cheo cha afisa mhusika.

Source: AAP