Mwongozo wa makazi: 5 muhimu kuhusu usalama mtandaoni

Kuna hatua za msingi ambazo, unaweza chukua kulinda taarifa zako binafsi na fedha mtandaoni.

Usalama mtandaoni

Usalama mtandaoni Source: Getty Images

1. Jikinge na kinga simu yako

Hakikisha unasimu yako kila mara. Kumbuka, kama simu yako haija fungwa na kama ime potea au imeibiwa, inaweza tumiwa kupata hela zako au kuiba utambulisho wako kwaku tumia taarifa ambazo ziko ndani ya simu yako.
https://www.staysmartonline.gov.au/mobile-devices
Protect your mobile device
Source: Getty Images
2. Kinga kompyuta yako

Unaweza jikinga kwaku pata ushauri kutoka kwa wataalam wanao aminika, punguza idadi ya maneno ya siri unayo tumia na tumia kinga thabiti mtandaoni. Hifadhi data zako katika hali salama kila mara, na hakikisha wanao hifadhi data hizo wana idhini yaku fanya hivyo.
 https://www.staysmartonline.gov.au/computers/secure-your-computers
Secure your computer
Source: Getty Images
3. Linda taarifa zako binafsi na siri zako

Kinga taarifa zako za siri jinsi unavyo kinga hela zako. Mtu anaweza tumia utambulisho wako, kupata mikopo kwa jina lako, kutumia kadi zako za benki, kudai mafao ya ustawi na hali hiyo inaweza haribu uwezo wako wakupokea mikopo.
Protect your privacy
Source: Getty Images


4. Usichangie neno lako la siri 

Tumia neno la siri laki pekee na usilichangie na watu wangine. Unaweza tumia mchanganyiko wa herufi, nambari zinazo zidi nane.

Protect your password
Concept stock photograph depicting Cyber Security theme, Thursday, April 28, 2016. Source: AAP/Dave Hunt



5. Hakikisha unatumia intanet salama

Intanet unayo tumia inaunganisha ulimwengu wa nje na kompyuta yako. Kama haija kingwa vizuri, mtu anaweza itumia kupata maelezo yako au kuiba kompyuta yako kwa ajili ya matumizi yake binafsi.
        
Secure your internet connection
Source: Getty Images



Kama unaamini siri zako zime vujwa, wasiliana na ofisi ya taarifa ya Australia kwa msaada kupitia namba hii ya simu: 1300 363 992.

Unaweza tazama orodha ya tisho zaki sasa za intanet pamoja na maneno yanayo tumiwa mtandaoni kupitia tovuti ya stay smart online: www.staysmartonline.gov.au  

Kwa makala ya ziada ya SBS Swahili kuhusu Mwongozo wa Makazi: tembelea tovuti hii:




Share

Published

Updated

By Ildiko Dauda
Presented by Gode Migerano


Share this with family and friends