1. Nchini Australia, mamlaka hugawanywa kati ya serikali ya taifa, mkoa na majimbo.

Source: AAP
2. Mara nyingi Nyumba ya Wawakilishi bungeni huitwa, Nyumba ya Chini, ina jumuisha wabunge wapatao 150 kutoka nchi nzima.
Nyumba hiyo huamua chama kitakacho unda serikali, pia hupitisha sheria, hufuatilia utendakazi pamoja naku jadili maswala yenye umuhimu kwa taifa. Baada ya uchaguzi mkuu, serikali huundwa na chama ambacho kina wabunge wengi ndani ya nyumba ya chini bungeni. Kiongozi wa chama chenye idadi kubwa yawa wakilishi ndani ya nyumba ya chini, ndiye huwa Waziri Mkuu.

Source: AAP
3. Seneti ama kama inavyo julikana mara nyingi, Nyumba ya Juu, ina jumuisha idai ya wanachama wapatao 76, kumi na mbili kutoka kila mkoa, na wawili kutoka majimbo mawili nchini. Jukumu kuu la Seneti niku chunguza miswada inayo tumwa kutoka Nyumba ya Chini ya bunge la taifa. Maseneta hu hudumu kwa mihula ya miaka 6, wakati nusu yama seneta huchaguliwa kila miaka mitatu ama katika uchaguzi mkuu.

Source: Getty Images
4. Serikali ya taifa la Australia hugawanywa katika vitengo vitatu: bunge, utawala na mahakama.
Bunge la Australia, lina jumuisha wawakilishi ambao wame chaguliwa kwa misingi ya demokrasia nchini kote. Wajibu wa bunge niku jadili nakupigia kura sheria mpya ambazo huwasilishwa chini ya mamlaka ya kitengo 51 cha Katiba.

Source: Getty Images

Source: AAP
Mahakama ni mkono wa sheria wa serikali, ni huru na tofauti na bunge na mamlaka. Jukumu lake niku hakikisha sheria za Australia zina fuatwa. Lazima pia ihakikishe mikono mingine ya serikali haikiuki mamlaka ya katiba.

Source: Getty Images
5. Nchini Australia serikali ya taifa huchaguliwa kupitia kura, ambayo ni lazima kwa kila raia.
Uchaguzi wa taifa hufanywa kila miaka mitatu. Uchaguzi mkuu ujao utafanywa katika vituo zaidi ya 8000 nchini kote, tarehe 2 Julai kuanzia saa mbili asubui hadi saa 12 jioni. Raia wa Australia wote, wenye umri wa miaka 18 na zaidi wanapashwa jiandikisha nakupiga kura.

Source: Getty Images