Mwongozo wa Makazi: Jinsi yaku pata huduma ya afya ya akili Australia

Nimuhimu kuwa na huduma za afya ya akili kama sehemu yaku wasaidia wakimbizi katika mchakato waku anza maisha mapya.

Mtaalam amshauri msichana

Mtaalam amshauri msichana Source: Picha: Getty Images

Wakimbizi wana athari kubwa yakuwa na matatizo ya afya ya akili kuliko umma pana ya Australia. Na unyanyapaa unao zingira ugonjwa wa akili, uhaba wa uelewa kuhusu huduma zilizopo pamoja na uelewa mdogo wa Kiingereza, unaweza fanya iwe vigumu kupata huduma ya afya ya akili.

Baadhi ya hatua zaku pata huduma bora ya afya ya akili zina jumuisha:

Tembelea Daktari wako au GP

Unastahili tembelea Daktari wako au GP, ambaye anaweza kufanyia uchunguzi naku andaa mpango wa matibabu wa afya ya akili. Unaweza tumwa kwa huduma za afya ya akili, kama wataalam wa akili, GP wako atakapo kupa mpango wa matibabu ya afya ya akili."
 Doctor with patient in hospital
Daktari akimuhudumia mgonjwa Source: Getty Images

Malipo toka Medicare

Malipo kutoka Medicare yanaweza patikana kwa huduma maalum za afya ya akili, zinazo tolewa nama GP, wataalam wa ugonjwa wa akili, wanasaikolojia, wafanyakazi wa jamii wanao fuzu pamoja na wataalam wa kazi. Unaweza rejea kumwona GP au mtaalam wa akili baada ya kupokea tiba mara sita, kulingana na mahitaji yako ya afya, kwa ajili yakupokea tiba zingne nne za ziada.
Medicare Debate
Kadi ya Medicare Source: AAP

Je naweza pokea huduma?

Unaweza hudumiwa kama una kadi ya Medicare na kama ume bainiwa una ugonjwa wa akili. Mradi wa serikali wa kwa huduma ya afya ya akili, hutolewa kwa "wagonjwa ambao imebainiwa wana ugonjwa wa akili, na wanaweza faidi kupitia mbinu ya muundo wa usimamizi wa mahitaji yao ya matibabu".

Hata hivyo kuna masharti mengine kwa wanao funikwa na mpango huo.


Kama unahitaji maelezo ya ziada kuhusu kama unaweza hudumiwa, kudai na mchakato wa malipo, unaweza pigia Medicare Australia kwa namba hii 132 011 au unaweza tembelea tovuti ya .

Naweza pata huduma ya wakalimani?

Interpreter in Health sector
Mkalimani katika sekta ya afya Source: SBS


Si vizuri kuzungumza kuhusu maswala nyeti ya afya ya akili katika lugha yakigeni. Hata hivyo, watalaam wa afya wame pendekeza usitegemea jamaa wako kuwa wakalimani wako, kwa sababu hiyo inaweza kuwa tatizo.

Hii ndio sababu kuna wakalimani. Madaktari wanaweza tumia wakalimani kupitia huduma ya ukalimani kwa simu au ana kwa ana, kwa hiyo zahanati inatarajiwa kutumia huduma hiyo kwa ajili yaku pata matokeo bora ya afya kwako.

Huduma za ushauri wa mateso

Refugee and migrant mental health in Australia
Refugee and migrant mental health in Australia. Source: AFP


Iwapo ime pitia mateso ambayo yana endelea kuathiri maisha yako, kuna huduma maalum za ushauri unazo weza tumia. STTARS ni shirika la shirika hili huwasaidia watu kutoka mazingira ya ukimbizi na uhamiaji, ambao wame pitia uzoefu wa mateso au wame sumbuliwa kwa sababu ya mateso, vurugu, vita au kufungwa kinyume na sheria kabla yaku wasili nchini Australia. STTARS hutoa zahanati ya afya ya akili kila wiki, inayo kuruhusu kupokea huduma ya wataalam wa akili katika mazingira ya jamii.

Huduma zingine ndani ya jamii

Migrant Refugee Resources
Rasilimali za wakimbizi na wahamiaji Source: Migrant Refugee Resources


Jamii yako na uhusiano waki jamiini muhimu kwa afya nzuri ya akili. Kuna huduma kadha zaki jamii ambazo zinaweza kusaidia. Kwa mfano , huandaa mikutano ambako vikundi vya walio wasili nchini hivi karibuni hupewa taarifa na maelezo ya jinsi yaku pokea huduma ya afya ya akili kwa ujumla, nakujaribu kuelewa mazingira hayo.

“Kama washiriki katika huduma za mitaa ambazo zinaweza saidia katika sehemu ya mchakato wauponyaji," kama alivyo sema Olivia Nguy ambaye ndiye

“Tunajua uzoefu katika nchi kama Australia, ambako watu wanaomba hifadhi na wakati wanasubiri matokeo ya maombi yao ya ukimbizi kushughulikiwa, yanaweza kuwa na matokeo mabaya kwa afya yao ya akili" kwa mujibu wa Samantha Ratnam, ambaye ndiye meneja wa huduma za wateja katika shirika la Asylum Seeker Resource Centre.

Kuna miradi maalum inayo jumuisha ushauri bila malipo ambayo unaweza tumia, kama unapitia viwango vya juu vya matatizo yaki saikolojia. Unaweza tumwa pia kwa vipimo vya akili na miradi ya matibabu.

(HSS) hutoa pia misaada inayo hitajika kwa wanao wasili kwa viza zaki binadam kwa muda wa mwaka mmoja baada yaku wasili kwao.

Viungo muhimu:

Kwa maelezo zaidi kuhusu miradi ya afya ya akili katika lugha yako tembelea:  

Asylum Seeker Resource Center's

Share

Published

Updated

By Ildiko Dauda
Presented by SBS Swahili
Source: SBS


Share this with family and friends