Tanzania ili orodheshwa katika Kundi F pamoja na Morocco, Zambia na DR Congo.
Katika mechi ya kwanza ya kundi hilo Morocco ilionesha ubabe wake kwa kuicharaza Taifa Stars magoli 3 bila jibu. Licha ya kichapo hicho, mamia yama shabiki wa Taifa Stars wanao ishi Australia, wali amkia mechi hiyo mapema kumshabikia Charles Kokola M'Mombwa aliye dhihirisha kuwa anastahili kiwango chakucheza dhidi ya wachezaji wa Morocco wenye majina tajika katika soka yakimataifa. Kupitia matokeo hayo hasi, sasa Tanzania lazima ioneshe viwango vya juu zaidi iwapo ina matumaini yaku fuzu kutoka kundi hilo.