Hata hivyo, majira ya joto nchini Australia yanaweza badilika haraka nakugeuka kuwa joto kali na hali ya ukame. Zaidi ya hiyo viwango vya juu vya miale ya UV, vinaomba umakini na kuzingatia.
Kwa hiyo, mtu anawezaje kuwa salama nakupata baridi, wakati wa joto kali katika msimu wa majira ya joto nchini Australia.
Katika hali ya hewa ya joto, kutokwa joto ni sehemu ya mchakato wa kawaida ambao miili yetu hupitia. Angelica Scott, ni GP mjini Sydney, amesema kutokwa jasho ni sehemu ya mfumo wa mwili wakusambaza joto na kudhibiti joto la mwili.
Hata hivyo, wakati wa hali ya hewa ya joto isiyo kawaida, mwili unaweza pitia mazingira mabaya sana kama, uchovu wa joto au, katika hali mbaya, kiharusi cha joto.
Uchovu wa joto hutokea wakati mwili, unapoteza viwango fulani vya chumvi na maji, mara nyingi kupitia kutokwa jasho.
Kwa upande mwingine, kiharusi cha joto ni hali mbaya zaidi. Huwa inazingatiwa kuwa ni dharura yakimatibabu kwa sababu, mwili hupoteza uwezo wakudhibiti joto yake ya ndani.