Baadhi ya mageuzi hayo yame thibitishwa tayari, wakati mengine yata fanyiwa uamuzi baadae.
Mageuzi hayo yanaweza wa athiri watu wengi wanao omba viza za kufanya kazi, kujiunga na wachumba wao na hata wazazi.
Kwa hiyo ni mageuzi yapi yanayo tarajiwa mwaka huu wa 2018?
Hata kama tuna fununu kuhusu mageuzi ya viza yanayo jiri mwaka huu, baadhi ya mageuzi hayo yanaweza badilishwa tena.
Iwapo unadhani unaweza athiriwa na mageuzi hayo, endelea kutembelea tovuti ya idara ya mambo ya ndani anwani yake ikiwa ni: www.homeaffairs.gov.au ambako utapata taarifa mpya kila mara.