Afrika Kusini imetoa kauli yakufungua vikao ambavyo vime anza katika kesi ambayo imewasilisha dhidi ya Israel. Vikao hivyo vya siku mbili vime jiri baada ya shutma za Afrika Kusini kuwa, Israel ina fanya mauaji yakimbari kwa kusudi katika kanda ya Gaza na, imeomba mahakama itoe amri maramoja yakusitisha shughuli zake zakivita.
Wakaaji wa Queensland wame onywa wajiandee kukabiliana na hali mbaya ya hewa, inayo jumuisha mvua nzito na uwezekano wa kimbunga. Wakati huo huo wakaaji wa baadhi ya sehemu za Magharibi Australia, wame onywa kuhusu joto kali linalo tarajiwa katika maeneo wanako ishi.
Waziri wa mambo ya ndani wa Burundi ametangaza kuwa serikali yake imefunga mipaka yake na Rwanda kuanzia Alhamisi. Martin Niteretse aliuambia mkutano aliokuwa akiuongoza katika jimbo la kaskazini mwa Burundi la Kayanza. Aliendelea kusema kuwa "tumefunga mipaka leo, yeyote anayesafiri hatavuka." Uamuzi huo unafuatia hotuba ya mwaka mpya ya Rais wa Burundi kwa taifa ambapo Evariste Ndayishimiye aliishutumu Rwanda kwa kuwa mwenyeji wa kile alichokitaja kuwa ‘’magaidi wa Burundi’’.
Msemaji serikali wa Somalia amesema Alhamisi kwamba serikali inafanya kila juhudi ili kuwaokoa abiria waliokuwa katika helikopta ya Umoja wa Mataifa iliyotekwa nyara na wanamgambo wa al Shaabab. Kila mbinu inafanywa ingawa mafisa wa kijeshi wamesema kwamba huenda ikawa vigumu kufika mahala walikopelekwa. Helikopta hiyo iliyokodishwa na UN ilikuwa ikipeleka dawa, wakati hitilafu za kimitambo zilipoilazimisha kutua kwa dharura karibu na kijiji cha Hindhere, kililochoko katikati mwa Somalia, na kinachodhibitiwa na wanamgambo.
Licha ya uhaba wa chakula unaoendelea, serikali ya Malawi mwezi uliopita ilipiga marufuku uagizaji wa mahindi ambayo hayajasagwa kutoka Kenya na Tanzania, kwa hofu ya kuenea ugonjwa “Necrosis” wa mahindi, au MLN. Ili kuwasaidia Wamalawi kupata chakula, shirika la mpango wa chakula duniani (WFP) limeanza kusaga tani 30,000 za mahindi ya msaada. Serekali inasema shehena ya kwanza ya nafaka iliyosagwa inatarajiwa kufika wiki ijayo. Cha kushangaza, mahindi ambayo WFP ilinunua na kuyasaga yanatoka Tanzania. Mahindi hayo yalishikiliwa wiki iliyopita, na kusubiri wataalam ili kuyapima kama yana ugonjwa.