Serikali ya shirikisho na jimbo zime toa msaada wa ziada kwa jumuiya zilizo athiriwa kwa moto wa vichaka mwaka jana katika maeneo ya Kusini Queensland. Tangazo hilo limejiri bada ya pambano kubwa la moto wa vichaka karibu ya Tara, kuharibu nyumba nyingi jimboni Queensland kuliko janga la Black Summer na ulidumu kwa siku 10 mwanzo wa Novemba mwaka jana.
Zaidi ya $200 milioni za uboreshaji wa nishati zinatarajiwa kusaidia kupunguza gharama ya bili za umeme, kwa zaidi ya nyumba elfu 30 za wapangaji waki jamii pamoja na wapangaji wengine jimboni New South Wales. Nyumba zilizo zeeka zilizo ezekwa vibaya pamoja na sehemu ambako wakaaji hupitia uzoefu mubaya wa joto na baridi yakupindukia, itakuwa kipaumbele katika maboresho ya nishati yaliyo tangazwa na serikali za shirikisho na jimbo la New South Wales.
Tanzania imesimamisha safari zote za ndege kutoka Nairobi hadi Dar es Salaam kuanzia Januari 22, 2024. Kwenye taarifa Jumatatu, Mkurugenzi Mkuu wa Halmashauri ya Kusimamia Safari za Ndege ya Tanzania (TCAA), Hamza Johari, alisema kuwa hilo linafuatia hatua ya Kenya kukataa ndege za kubeba mizigo kutoka shirika la ndege la Air Tanzania kusafiri nchini. Hatua hiyo inaonekana kufufua tofauti za kimahusiano ambazo zimekuwepo baina ya Kenya na Tanzania kwa muda mrefu.
Naibu Rais Rigathi Gachagua amesema atawasilisha kesi kuishinikiza Tume ya Huduma za Mahakama (JSC) kumwondoa Jaji Esther Maina katika Idara ya Mahakama, kwa madai ya ufisadi na matumizi mabaya ya mamlaka. Akizungumza Jumapili, Januari 14, 2024 mjini Iten, Kaunti ya Elgeyo Marakwet, katika ibada ya kanisa iliyokuwa imehudhuriwa na Rais William Ruto, Bw Gachagua alisema Jaji Maina alitangaza kwamba alipata mali yake kwa njia haramu, bila ya kumpa nafasi yoyote kujitetea. Bw Gachagua alisema kuwa atawasilisha malalamishi yake kwa JSC, Alhamisi (Januari 18, 2024), saa 8.15 alasiri.