Sheria zinazo zuia uchochezi wa vurugu jimboni New South Wales, zita fanyiwa tathmini wakati kuna ongezeko ya mivutano kati ya jumuia jimboni humo kwa sababu ya mgogoro wa Israel-Hamas. Baadhi ya vikundi vya jumuiya vina wasiwasi kuwa sheria zinazo zuia uchochezi wa vurugu hazitoshi, hali ambayo imesababisha tathmini kutoka kwa hakimu mkuu wa zamanai wa mahakama kuu ya New South Wales, Tom Bathurst AC KC. Kiongozi wa jimbo hilo Chris Minns amesema ni muhimu kuwa na kinga yakisheria kwa watu kutoka jumuiya mbali mbali za dunia zinazo ita NSW nyumbani.
Ongezeko kwa visa vya picha chafu kutumiwa kuwalaghai vijana, zime sababisha onyo kwa wazazi na walezi wakati wanafunzi wanarejea darasani. Sextortion ni tendo ambako wahalifu huwadanganya au kulazimisha mtu kutuma picha zao wakiwa uchi kabla yakutisha kuchangia picha hizo kama masharti yao hayata timizwa. Visa vya matukio haya vina ongezeka na jeshi la polisi la shirikisho la Astralia, lime onya kuhusu madhara makubwa ya kiwewe kwa walengwa.
Wawili kati ya wagombea wakuu wa upinzani kwenye uchaguzi wa Disemba mwaka jana nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wameitisha maandamano Jumamosi, wakati wa kuapishwa kwa Rais Felix Tshisekedi kuongoza muhala wa pili. Tshisekedi alishinda kwa kishindo uchaguzi wa tarehe 20 Disemba, lakini uchaguzi huo uligubikwa na madai mengi ya udanganyifu, changamoto za kiufundi na kasoro nyingine. Viongozi wawili wa upinzani, Martin Fayulu na Moise Katumbi pamoja na wapinzani wengine, waliomba uchaguzi mpya, ombi ambalo lilitupiliwa mbali na serikali.
Kiongozi wa upinzani nchini Uganda na mgombea wa zamani wa urais Bobi Wine leo Alhamisi amesema polisi waliizingira nyumba yake na kumuweka “chini ya kizuizi cha nyumbani” kabla ya maandamano yaliyokuwa yamepangwa kufanyika. Wanasiasa wa upinzani walikuwa wamepanga maandamano dhidi ya barabara mbovu sana nchini Uganda, ambayo ni mwenyeji wa mikutano miwili ya kimataifa katika siku zijazo. Mgombea wa zamani wa urais Kizza Besigye wa chama cha upinzani cha Forum for Democratic Change amesema leo kuwa yeye pia hakuruhusiwa kuondoka nyumbani kwake.
Spika wa Seneti Amason Kingi Alhamisi, Januari 18, 2024 alipata pigo kuu kisiasa baada ya waanzilishi wa chama chake cha Pamoja African Alliance (PAA) kuhamia chama cha ODM. Kinara wa Upinzani Raila Odinga aliwapokea wanachama hao wa PAA na kuwakaribisha rasmi ndani ya chama chake. Hafla hiyo ilifanyika katika makao makuu ya ODM, Chungwa House, Nairobi.