Taarifa ya Habari 23 Januari 2024

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Kuna taarifa serikali ya shirikisho inazingatia uwezekano wakurekebisha mpango wake wa awamu ya tatu ya makato ya kodi, muswada huo utakapo wasilishwa mbele ya baraza la mawaziri hii leo.


Mamlaka ya dharura jimboni Queensland, wana fuatilia wa dhoruba inayo undwa, ambayo inatarajiwa kugonga eneo la kaskazini kama kitengo cha tatu cha kimbunga.

Makundi ya biashara yame sema yana unga mkono pendekezo lakuongeza idadi ya wiki zinazo tolewa chini ya mfumo wa likizo ambayo wazazi hulipwa kwa ajili yamalezi ya watoto.

Siku ya Jumatatu Cameroon imekuwa nchi ya kwanza kuanzisha mpango wa kawaida wa utoaji chanjo ya malaria kwa watoto. Ugonjwa wa maralia unasababishwa na vimelea vya mbu unaosambaa baada ya kung’atwa na mbu mwenye malaria. Mara nyingi watu huwa na dalili za mafua na kama haukutibiwa, unaweza kusababisha madhara makubwa ikiwa ni pamoja na kifo.

Mkutano mkuu wa kundi la mataifa ya G77 umemalizika mjini Kampala, baada ya mjadala wa haja ya mabadiliko kwa upande wa taasisi za kimataifa za kifedha kuhusiana na utoaji mikopo na ulipaji madeni. Lengo ni kujikwamua kutoka minyororo ya utegemezi wa misaada ya maendeleo ambayo huandamana na masharti makali kutoka kwa mataifa tajiri wafadhili.

Tume Huru ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (CENI) ilitangaza matokeo ya muda ya uchaguzi wa wabunge wa mikoa usiku wa Jumapili ikiwa ni zaidi ya mwezi mmoja tangu kura kupigwa. Watu 688 ndio walichaguliwa kuwa wabunge wa mikoa kati ya 780 nchini humo. Idadi itaongezwa baada ya baadhi ya changamoto kutatuliwa katika baadhi ya maeneo. Matokeo yaliyotangazwa haya husu baadhi ya maeneo kama Budjala mkoani Ubangi Kusini, Bomongo na Makanza mkoani Equateur ambako uchunguzi bado unaendelea kutokana na hitilafu za uchaguzi.

Katika michezo, tegemeo la Australia katika michezo ya wazi ya tennis ya Australia atupwa nje ya michuano, Socceroos kumkosa nyota mshambuliaji wake katika kombe la Asia, na wenyeji watupwa nje ya michuano katika kombe la Afrika.




Share