Kampeni za Urais nchini Kenya zime anza sasa kwa kina, baada ya vinara wa miseto kutangazwa rasmi siku chache zilizo pita. Naibu Rais wa Kenya Dr William S Ruto, ata kabiliana na wandani wake wa zamani Raila Odinga taifa hilo liki jiandaa kuingia debeni hivi karibuni.
Katika hafla iliyo andaliwa ndani ya ukumbi wa michezo wa Kasarani mjini Nairobi, Kenya, Bw Ruto alipewa idhini rasmi yaku peperusha bendera ya mseto wa UDA katika uchaguzi mkuu. Na katika hotuba yake yaku kubali fursa hiyo Bw Ruto aliweka wazi vipaumbele vya mseto wake utakapo shinda uchaguzi mkuu.
Bonyeza hapo juu kwa taarifa kamili.