Wataalam wa elimu huwa hamasisha wazazi na walezi wahusike katika elimu ya wanao.
Hizi hapa mbinu unaweza tumia kumsaidia mwanako, kuwa na uzoefu mzuri shuleni.
Husika kwa hali chanya katika elimu ya mwanako
Ni muhimu kuhakikisha mwanako anaenda shuleni kila siku. Kuwa shuleni kunaweza kuwa na ushawishi chanya
Unda mazingira yanayo msaidia mwanako kufika shuleni bila wasi wasi wala mafikara mengi.
Pata taarifa kuhusu shule yake na endelea kuhusika
Nivizuri kujizoeza mazoea ya kawaida ya shule za Australia kama, umuhimu waku mwandalia mwanako chakula cha mchana au, kumchukua shuleni kwa wakati. Pia kuna shughuli unaweza fanya nje ya shule ambazo, zinaweza msaidia mwanako, unaweza zungumza kuhusu shule, nakumwuliza walivyo jifunza, au kuwauliza walicho furahia siku hiyo.
Wahimize wasome
Msomee kitabu mwanako mara kwa mara, au mwambie akusomee kitabu hicho. Hata hivyo, nivizuri kuweka matarajio ambayo yanaweza fikiwa. ili pata kuwa, vijana ambao wazazi wao husoma vitabu pamoja nao katika mwaka wao wa kwanza wa shule ya msingi, walikuwa na matokeo mazuri zaidi kuliko wanafunzi ambao, wazazi wao hawakusoma vitabu hivyo nao au walifanywa hivyo mara moja moja.

Research has found that the more devices a child had access to, the less they read in general. Source: LightRocket
Husika katika mikutano ya walimu na wazazi
Kuhudhuria , ambayo huwa mara mbili kwa mwaka ni mbinu nzuri yaku husika katika shughuli za shule. Katika mikutano hiyo, mzazi hupata fursa yakuzumza na mwalimu wakiwa pekee yao.
Ni fursa yaku kutana na mwalimu wa mwanako pamoja nakujenga uhusiano chanya na shule ya mwanako. Unashauriwa kuhudhuria mahojiano hayo ukiwa tayari kuwa wazi katika mazungumzo hayo.
Shule nyingi hutoa msaada wa wakalimani, kulingana na utofauti wa jamii.

A survey says schools are leaning on fundraising and teachers are paying for classroom supplies. (AAP) Source: AAP
Jitolee katika shughuli za shule ya mwanako
Kuhusika katika maisha ya shule ya mwanako ni zaidi ya kuhudhuria mikutano. Unaweza jitolea kuwasikia watoto wakisoma darasani, kuwasaidia katika michezo, katika sehemu ya maakuli au shambani. hiyo ni njia nyingine yaku shiriki shuleni.
Maelezo ya ziada
inamaelezo kuhusu jinsi yaku husika katika elimu ya mwanako na mifumo tofauti ya shule nchini Australia.
Kuhusiana: Testing Teachers itaoneshwa Jumatano, 19 Aprili saa 2.30 usiku kwenye runinga ya SBS na kipindi hicho kinaweza patikana baadae kwenye mtandao wa SBS On Demand. Tazama kionjo hapa chini: