Mwongozo wa makazi: Hatua 3 zakupata huduma ya afya ya akili kupitia Medicare

Kupitia mfumo wa Better Access initiative, wagonjwa wanaweza pata marupurupu ya Medicare kwa baadhi ya huduma za afya ya akili, zinazo tolewa na madaktari, wataalam wa saikolojia, wataalam wa saikatria, wafanya kazi wa jamii na wataalam wengine.

Male doctor writing in patient chart mid section

Male doctor writing in patient chart, mid section Source: AAP

1.Tembelea daktari wako kwa uchunguzi wa afya yako.

Daktari wako anaweza kuandalia "Mpango wa matibabu wa Afya ya Akili". Marupurupu ya Medicare yanaweza patikana mara kumi kwa mwaka, unapo tumia huduma ya afya ya akili.

2. Pata rufaa

Kama Daktari wako ame kuandalia mpango wa matibabu, unaweza tumwa kwa wahudumu wa afya ya akili, kama wataalam wa saikatria.

 
Mental health at work by AAP
Mental health at work by AAP Source: AAP

3. Fuatilia

Unaweza rudi kumwona daktari au mtaalam wa saikatria anaye kutibu baada yaku mwona mara sita ama kulingana na mahitaji yako ya afya. Daktari wako na mtaalam wa saikatria wanaweza kutuma opokee matibabu ya ziada mara nne.

Psychologist
Source: Public Domain


Nani anastahili kupokea huduma hii?

Kila mtu ambaye ana Medicare na ime bainiwa kuwa ana ugonjwa wa akili. Mfumo wa Better Access hauwezi tumiwa kwa magonjwa kama kuweweseka, matumizi ya tumbaku machafuko na matatizo ya kiakili.
Kwa maelezo ya ziada tembelea: Better Access initiative. Maelezo kuhusu anayestahili kupokea huduma hii, kudai na michakato ya malipo inaweza patikana kutoka Medicare Australia, namba ya simu 132 011 Unaweza pata mengine hapa pia: Better access to mental health care fact sheet
More on mental health support

Jinsi yakupata huduma za afya ya akili



Share

Published

Updated

By Ildiko Dauda, Olga Klepova
Presented by Gode Migerano
Source: SBS Radio


Share this with family and friends