Jinsi yakupata huduma za afya ya akili

AAP

AAP Source: AAP

Ugonjwa wa akili uko katika nafasi ya tatu katika orodha ya magonjwa yanayo waathiri wa Australia, magonjwa yanayo piku ugonjwa wa akili katika orodha hiyo ni saratani na ugonjwa wa moyo. Hata hivyo, takwimu zina onesha kuwa viwango vya wanao tumia huduma ya afya ya akili ni ndogo sana miongoni mwa jumuiya zawa hamiaji. Uelewa mdogo kuhusu huduma zilizopo, unyanyapaa wakiutamaduni, na matatizo ya lugha mara nyingi huwazuia kuomba msaada.



Share