Key Points
- The AEC provides tools to help you find your electorate and polling centre.
- Multiple voting options are available before and on election day.
- Voting information is available in multiple languages.
- The AEC provides a telephone interpreter service to help you cast your vote.
Australia ina tume huru inayo simamia mfumo wa uchaguzi. Ni wajibu wa Tume ya Uchaguzi ya Australia (AEC) kuhakikisha raia wanao stahiki wanaweza piga kura na kusaidia kuunda serikali yetu ya shirikisho.
Tambua eneo bunge lako
Kuna maeneo bunge ya shirikisho 150 nchini Australia. AEC
hutoa kifaa cha mtandaoni cha kukusaidia kutambua eneo bunge unako ishi. Kujua eneo bunge lako, tembelea .
Pata kituo chako cha kupigia kura
AEC husimamia maelfu ya vituo vya kupiga kura. Shule, vituo vya jumuia na kumbi za kanisa kawaida hutumiwa kama vituo vya kupigia kura katika siku ya uchaguzi.
“Ni rahisi kupata kituo cha kupiga kura kilicho karibu yako,” Msemaji wa AEC Jess Lilley amesema.
“Utaweza andika jina la kitongoji au namba ya kitongoji chako na, kifaa chetu kita kusaidia kupata wagombea wa eneo bunge lako na sehemu unaweza piga kura.”
Namna rahisi ya kupiga kura nikutembelea kituo chakupiga kura unako ishi katika siku yakupiga kura, ambayo daima huwa Jumamosi.
Timu za maafisa wauchaguzi wanao safiri hutembelea vituo vya huduma za wazee, jumuiya za vijijini, hospitali na magereza.

Election corflute signs are seen at the polling booth for the Werribee by-elections at Werribee in Melbourne. Source: AAP / DIEGO FEDELE/AAPIMAGE
Piga kura katika lugha yako
Mtu anaweza kusindikiza kama unahitaji msaada. inaweza patikana pia kukusaidia kupiga kura katika lugha yako.
Njia zingine zakupiga kura
Vituo vya kupiga kura mapema hufunguliwa wiki kadhaa kabla ya siku ya uchaguzi mkuu.
Kupigia kura katika jimbo lingine na ng'ambo
Hakuna tatizo kama unampango wakuwa katika jimbo lingine. Unaweza tumia kura ya posta au tembelea kituo chakupigia kura katika jimbo lingine.
Unaweza piga kura pia ukiwa ng'ambo. zinaweza patikana katika tovuti ya AEC, pamoja na chaguzi zinazo shughulikia mazingira yako binafsi. Baadhi ya Balozi za Australia hutoa vituo vya kupigia kura.

A dog stands as voters cast their ballots at a polling station during a federal election in Sydney, Australia, on Saturday, May 18, 2019. Credit: Bloomberg/Bloomberg via Getty Images
Usambazaji wa taarifa
Vyama vya kisiasa na wabunge huru husambaza taarifa nje ya vituo vya kupigia kurat. Ila, usi ache wakupotoshe, mchambuzi wa uchaguzi William Bowe amesema.
“Vyama hugawa ‘kadi za jinsi ya kupiga kura’ katika vituo vya kupiga kura zinazo pendekeza ujaze karatasi yako yakura namna fulani. Si lazima upige kura hivyo, ni pendekezo tu.”
Piga kura yako
Utapokea karatasi moja ya kijani na nyingine nyeupe.
Karatasi ya kura ya Kijani
Karatasi ya kura ya kijani, ni ya kuchagua mgombea mmoja katika eneo bunge lako ajiunge na nyumba ya wawakilishi (nyumba ya chini bungeni).
Kuna viti 150 ndani ya Nyumba ya Wawakilishi, wanao wakilisha kila eneo bunge. Chama kinacho shinda viti vingi zaidi ndani ya Nyumba ya Chini huwa kina unda serikali.
“Wakati kawaida watu huwa wanafikiria kuhusu uchaguzi kwa maana ya kumchagua kiongozi wa taifa [Waziri Mkuu] atakuwa kiongozi wa chama kinacho shinda viti vingin bungeni, kwa hiyo hauta mpigia kura kiongozi huyo moja kwa moja,” Bw Bowe amesema.
Kupiga kura katika karatasi ya kijani, una stahili andika namba ‘1’ kando ya mgombea unaye pendelea, kisha namba ‘2’ kando ya jina la chaguo lako la pili na unastahili endelea hivyo hadi visanduku vyote katika karatasi hiyo vinajazwa namba.
Karatasi Nyeupe ya kura
Karatasi nyeupe ya kura hutumiwa kuchaguwa moja kati ya wagombea 76 ndani ya Seneti (Nyumba ya Juu). Utapiga kura kumchagua seneta kutoka jimbo au wilaya yako.
Kura ya Seneti huwa tofauti kidogo. Muenekano wa karatasi hiyo kubwa ya kura unaweza tisha, kwa sababu ina jumuisha wagombea wote katika jimbo lako.
“Ila kupiga kura kunaweza kuwa rahisi sana,” Bw Bowe ame elezea.
“Kuna njia mbili unaweza fanya. Kuna boxi juu ya mstari na boxi chini ya mstari. Juu ya mstari kuna moja ya kila chama. Njia rahisi na haraka zaidi yakupiga kura ni kuchagua vyama sita unavyo pendelea na uweke namba moja hadi sita kulingana na upendeleo wako. Kama una upendeleo fulani kuhusu wagombea unao taka pigia kura, unaweza weka namba katika boxi nyingi zaidi chini ya mstari. Ukipiga kura chini ya mstari, lazima uweke namba katika angalau boxi 12.”
Kuweka namba katika boxi katika orodha unayo penda, kuna lengo laku hakikisha kura yako ina enda mbali zaidi. Hali hiyo ina itwa ‘kura ya upendeleo’.
“Kama mtu ambaye ume mpa kura yako ya kwanza ana ondolewa katika hesabu, kura yako ita enda kwa mgombea mwingine unaye pendelea, na ita endelea hivyo hadi kura kura zote zina hesabiwa,” msemaji wa AEC Evan Ekin-Smyth amesema.

A ballot box is seen inside the voting centre at Collingwood in Melbourne, Saturday, October 14, 2023. Credit: CON CHRONIS/AAPIMAGE
Kura zisizo rasmi
Hakikisha unafuata maelekezo ya kupiga kura kwa makini. Kama karatasi yako yakupiga kura haija jazwa vizuri, itakuwa ‘kura isiyo rasmi’ na haita hesabiwa kwa matokeo ya uchaguzi.
Nini hufanyika kama haupigi kura?
Kupiga kura ni lazima. Sababu halali za kutopiga kura huwa kwa busara ya AEC ambao wata chunguza sababu ulizo toa. AEC ina elewa kuwa baadhi ya watu ambao wako ng'ambo kwa mfano huenda wasi weze piga kura.
“Kama mtu ambaye amesajiliwa hapigi kura, anaweza pea notisi ya kuto piga kura,” Bw Ekin-Smyth ame elezea.
“Kama unasababu halali, hiyo ni sawa. Tu arifu. La sivyo, uta lipa faini ya $20. Kama hatupati jibu, unaweza fikishwa mahakamani naku pewa faini ya $170 pamoja na gharama za mahakama.”
Hata hivyo, adhabu halisi ni kukosa kutoa usemi wako, kwa hiyo daima, fanya utafiti na enda kupiga kura.
Sajili ya taarifa potofu ya AEC
AEC ni huru na haina upendeleo, na mchakato wa uchaguzi ni mgumu sana. AEC imezindua kushungulikia taarifa za kupotosha na kudanganya zinazo zingira mchakato wa uchaguzi wa Australia.
Pata taarifa zaidi kuhusu jinsi yakupiga kura katika tovuti hii au piga simu kwa namba hii 13 23 26.
Makala haya yali tengezwa mara ya kwanza katika mwaka wa 2022. Ukweli wake ume chunguzwa na kusasishwa.
Jiandikishe au fuata makala yaliyo rekodiwa ya Australia Explained kwa taarifa za ziada na maelezo muhimu kuhusu kuanza maisha yako mapya nchini Australia.
Una maswali yoyote au mawazo ya mada? tutumie barua pepe kwa [email protected]