Mwongozo wa Makazi: 5 muhimu kuhusu ugonjwa wa akili kwa wahamiaji

Ingawa ugonjwa wa akili huathiri zaidi wazee, si sehemu ya kawaida ya kuzeeka. Utambuaji wa mapema huboresha maisha yawatu wanao athiriwa na ugonjwa wa akili pamoja na familia zao. Hata hivyo, wagonjwa kutoka jumuiya za tamaduni tofauti, hukabiliana na changamoto za ziada kupata utambuaji wa mapema na huduma inayo timiza mahitaji yao.

Elderly person

Elderly person Source: Public Domain/Pixabay

1. Uhaba wa elimu kuhusu ugonjwa wa akili na dalili zake.

Katika baadhi ya jumuiya, mtazamo kuhusu ugonjwa wa akili unadhaniwa kuwa ni ugonjwa wa akili, ugonjwa wa akili, sehemu ya kawaida ya kuzeeka au hata kutokuwa na maana yoyote. Ugonjwa wa akili husababishwa na mchanganyiko wa magonjwa ya ubongo yanayo athiri kumbukumbu, jinsi yaku fikiria, tabia na uwezo waku fanya shughuli za kila siku.

Brain scan
Female doctor holding CAT scan Source: AAP

2. Mtazamo wa ugonjwa wa akili kama sehemu ya kawaida ya kuzeeka.

Katika baadhi ya jumuiya, ugonjwa wa akili huchukuliwa kama sehemu ya kawaida ya kuzeeka. Utambuaji waku chelewa kwa ugonjwa wa akili mara nyingi huja hali ikiwa tete, kwa sababu ya uhaba wa elemu kuhusu dalili za mapema, sehemu yaku pata msaada, kuona haya au kubandikwa jina.

Carer with patient
Source: AAP

3. Unyanyapaa unao husishwa na ugonjwa wa akili

Watu wengi wahapendi kujadili ugonjwa huo kwa uwazi kwa sababu ya wasi wasi waku itwa 'wendawazimu'. Matokeo yake ni kwamba, huwa hawashiriki katika shughuli na watu wengine, au katika makundi yaki jamii.

Elderly lady
Source: Public Domain/Pixabay

4. Matatizo ya mawasiliano yanayo sababishwa na viwango duni vya elimu katika Kiingereza.

Mtu anapo kabiliwa na ugonjwa wa akili, baadhi ya watu wanaweza poteza ujuzi wanao wakiingereza, hali ambayo huwalazimisha kutumia lugha zao za asili.

Elderly people
Source: Pedro Ribeiro Simoes CC BY 2.0

5. Dhana kuwa wagonjwa hu hudumiwa na familia zao.

Katika baadhi ya jumuiya kuna hisia kuwa familia au watoto wata wahudumia wazazi ambao wana ugonjwa wa akili. Hata hivyo, maadili yakitamaduni yanapo changanywa na maadili mapya ya Australia, hali halisia kwa wazee wengi inabadilika.

Isolation
Source: Getty Images

Huduma za ushauri zinaweza patikana kwakupigia simu, huduma yaki taifa ya ugonjwa wa akili. Namba yao ni: 1800 100 500.

Kama unahitaji mkalimani, unaweza wasiliana na huduma yaki taifa ya ugonjwa wa akili kupitia simu. Pigia huduma ya wakalimani kwa simu ama TIS kwa ufupi. Namba yao ni: 131 450.


Share

Published

Updated

By Ildiko Dauda
Presented by Gode Migerano


Share this with family and friends