Jamii zawahamiaji zasherehekea kufeli kwa jaribio la mageuzi ya sheria za uraia bungeni

Malcolm Turnbull (kushoto) na Peter Dutton (kulia) waki wasilisha muswada mapema mwaka huu

Malcolm Turnbull (kushoto) na Peter Dutton (kulia) waki wasilisha muswada mapema mwaka huu Source: AAP

Jamii toka tamaduni tofauti zime pokea kwa shangwe uamuzi wa Seneti waku zuia pendekezo laku fanyia mageuzi sheria ya uraia, ambalo lili feli kujadiliwa kwa wakati ulio faa ndani ya seneti ya taifa.


Mageuzi hayo yange ongeza muda waku subiri kwa wakazi wenye viza zaku dumu kuwasilisha maombi ya uraia pamoja naku fanya mitihani ya kiingereza kuwa ngumu zaidi.

Mageuzi hayo yange mpa mamlaka ya ziada waziri wa uhamiaji, kama sehemu yaku fanya iwe vigumu kwa wahamiaji au wakimbizi kuwa raia wa Australia.


Share