Taarifa ya Habari 22 Aprili 2025

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS / SBS Swahili

Zaidi ya idadi yawa katoliki milioni 5 nchini Australia wana omboleza, kufuatia kifo cha Papa Francis. Imeripotiwa kuwa Papa alifariki akiwa na miaka 88, baada yaku kumbwa kwa kiharusi na mshtuko wa moyo.


Muda una anza kuwa adui wa baadhi ya wagombea wa uchaguzi mkuu, kuuza sera zao kubwa baada ya wa Australia kuanza kupiga kura zao katika uchaguzi mkuu wa shirikisho.

Mazungumzo kati ya serikali ya DRC na waasi wa AFC/M23 yanaripotiwa kuendelea jijini Doha nchini Qatar. Licha ya vyanzo kutoka katika muungano wa waasi wa AFC/M23 na upande Joseph Kabila kuripoti kwamba rais huyo wa zamani wa DRC alitembelea Goma Ijumaa ya wiki hii, Marekani inasema inaendelea na juhudi zake kupunguza mzozo wa sasa.

Bonyeza hapo juu kwa taarifa kamili.

Share