Kiongozi wa New South Wales Chris Minns, amesema nguvu kamili ya sheria itatumiwa kuchunguza tisho la mtandaoni dhidi ya msikiti mmoja wa Magharibi Sydney. Msikiti wa Lakemba ume omba hatua thabiti ichukuliwe dhidi ya unyanyasaji wa waislamu, baada ya mtu mmoja kuchapisha maoni katika mtandao wa TikTok, akidokeza shambulizi la 2019 ndani ya msikiti wa Christchurch nchini New Zealand ambako watu 51 wali uawa. Jeshi la Polisi la New South Wales, lime anza uchunguzi kwa tisho hilo.
Kiwango cha ukosefu wa ajira nchini Australia, kime baki imara licha ya kushuka kwa kasi kwa idadi ajira. Ofisi ya takwimu ya Australia imesema kiwango kinasalia kuwa asilimia 4.1 katika mwezi wa Februari licha ya takriban ajira elfu 53,000 kupotezwa kutoka uchumi kwa zaidi ya mwezi na makubaliano ya utabiri ya ongezeko la kupata ajira ni elfu 30,000.
Imesema kiwango kimesalia hivyo kwa sababu ya idadi ya watu ambao hawana ajira kupungua kwa elfu 11,000, na viwango vya ushiriki kupungua kwa asilimia 0.4 hadi asilimia 66.8.
Bw Albanese amejibu ripoti kuwa sekta ya madawa ya Marekani, ime maafisa wa serikali ya Trump, kuweka ushuru kulipiza kisasi kwa inacho dai ni sera za uharibifu za bei za Australia, chini ya Mpango wa Faida za Dawa. Utafiti wa madawa na watenenezaji wa Marekani, wame wasilisha lalamishi rasmi kwa mwakilishi wa Biashara wa Marekani Jamieson Greer, ikiomba serikali ya Trump ichukue hatua thabiti, wakisisitiza kuwa mfumo wa PBS unafeli kutambua thamani ya ubunifu wa Marekani.
Waasi wa M23 wauteka mji wa Walikale licha ya mwito wa amani. Hayo yanajiri siku moja tu baada ya Marais wa Kongo na Rwanda kukutana na kuonyesha niya yakuweko na usitishwaji mapigano huko mashariki mwa Kongo. Taarifa kutoka Walikale zinasema waasi wa M23 waliuteka mji huo Jumatano jioni baada ya milio ya risasi ya hapa na pale. Mmoja ya viongozi wa jadi wa mji wa Walikale amesema waasi hao walipenyeza ngome ya jeshi na kutumia njia mbadala kuufikia mji huo. Mji wa Walikale ni watatu kwa uzalishaji wa madaini ya bati ulimwenguni. Na umekuwa mji wa kimkakati ambao unaunganisha majimbo manne ya mashariki mwa Kongo yakiwemo : Kivu Kaskazini, Kivu Kusini, Tshopo na Maniema.
Abiy Ahmed amesema serikali yake haitafuti mzozo na taifa jirani lililo hasimu wa siku nyingi, Eritrea, baada ya maafisa kadhaa kwenye mataifa ya kanda hiyo kutoa hadhari kuwa nchi hizo mbili huenda zinaelekea kupigana vita. Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed ameandika kwenye ukurasa wa mtandao wa X kuwa nchi yake haina dhamira ya kujiingiza kwenye mzozo na Eritrea kwa lengo la Ethiopia kujipatia nafasi ya kuifikia Bahari ya Shamu. Eritrea inaituhumu Ethiopia, taifa lisilo na bandari kuwa inaimezea mate bandari yake ya Assab katika juhudi za serikali mjini Addis Abbaba kuifikia bahari ya Shamu.
Mkataba wa ushirikiano ambao Kiongozi wa ODM Raila Odinga alitia saini na serikali ya Kenya Kwanza unaendelea kuzaa matunda huku washirika wake wakinufaika na nyadhifa za makatibu wa wizara. Katika mabadiliko ambayo Rais William Ruto alifanyia makatibu wa wizara Alhamisi, Machi 20, 2025, washirika wa Bw Odinga waliteuliwa kuhudumu katika Idara za wizara muhimu.