Australia imewapokea nakutoa hifadhi kwa makumi yama elfu ya wakimbizi kutoka sehemu zote za dunia.
Asilimia kubwa ya watu wanao zungumza Kiswahili nchini Australia, waliwasili nchini kama wakimbizi hata hivyo uzoefu wao unatofautiana.
Katika sehemu ya makala maalum ya Wiki ya Wakimbizi, SBS Swahili ilizungumza na balozi wa shirika la Refugee Council of Australia (RCOA) Bi Abang Anade Othow aliye changia nasi uzoefu wake, wakuwa mkimbizi pamoja na miradi anayo simamia kuboresha maisha yawatu ambao wanaishi katika mazingira magumu.
Kwa taarifa zaidi kuhusu RCOA, bonyeza hapa chini: