Wanaharakati wa waomba hifadhi, waonya kukaza kwa masharti ya misaada kuna athari kubwa

Mkurugenzi Mkuu wa ACOSS Cassandra Goldie akizungumza na waandishi wa habari nje ya bunge la taifa mjini Canberra, Australia

Mkurugenzi Mkuu wa ACOSS Cassandra Goldie akizungumza na waandishi wa habari nje ya bunge la taifa mjini Canberra, Australia Source: AAP

Wanaharakati wanao tetea maslahi ya waomba hifadhi, wame kosoa hatua za serikali ya shirikisho zaku endelea kukaza masharti yaku fuzu kushiriki katika mradi waku tatua huduma ya msaada.


Mradi huo hutoa kinga inayo jumuisha malipo ya chini ya dola 35 kwa siku, pamoja nakupokea msaada kutoka kwa afisa anaye shughulikia kesi yako. Huduma hiyo hutolewa kwa wanao subiri taarifa kuhusu hali yao ya uhamiaji.

Hata hivyo, idara ya maswala ya nyumbani imesema kupitia kauli kuwa hatua hiyo si mradi wa msaada wa ustawi wa jamii.

Idara hiyo ime ongezea kuwa mradi huo ume undwa kutoa msaada kwa muda mfupi, kwa wanao thibitisha kuna vizuizi kutatua hali yao ya uhamiaji.

Kauli hiyo imeongezea kuwa watu ambao wako nchini kwa viza za mpito na wana ruhusa yakufanya kazi na wanauwezo wakufanya kazi, wanatarajiwa kujitegemea wakati hatma ya viza yao inatatuliwa.

Kwa mujibu wa kauli ya idara ya maswala ya nyumbani, tathmini yakufuzu kwa wanao pokea msaada huo inaendelea na hakuna mtu ambaye ame zuiwa kupokea msaada toka mradi huo kwa sababu ya mchakato wa tathmini hiyo.


Share