Australia yabadilisha msimamo wa miaka 20 kwa uvamizi wa Israel katika maeneo ya Palestine

UN-ISRAEL-PALESTINIAN-DIPLOMACY-CONFLICT

A screen shows the results of the vote on the resolution entitled "Peaceful settlement of the question of Palestine" at the General Assembly 46th plenary meeting on December 3, 2024, at the UN headquarters in New York City Source: AFP / KENA BETANCUR/AFP via Getty Images

Australia imebadilisha msimamo wayo kwa azimio la Umoja wa Mataifa, linalo taka Israel isitishe kukalia kwa mabavu maeneo ya wapalestina.


Ni mara ya kwanza katika zaidi ya miongo mbili, Australia ime unga mkono pendekezo hilo ndani ya Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa.

Idadi ya majeruhi inapo endelea kuongezeka katika vita mjini Gaza, msimamo wa Australia unabadilika kwa hoja ya Palestine kuwa nchi huru.

Mara ya mwisho Australia ilipiga kura kuunga mkono Israel kuondoka katika maeneo yawa Palestina ilikuwa katika mwaka wa 2001.

Tangu wakati huo, Australia ilikuwa ime amua kuto piga kura- hadi sasa.

Share