Chama cha Labor chatumia matokeo ya chaguzi ndogo kumwongezea Turnbull shinikizo

Bill Shorten na Susan Lamb washerehekea ushindi wa chaguzi ndogo ya 'Super Saturday'

Bill Shorten na Susan Lamb washerehekea ushindi wa chaguzi ndogo ya 'Super Saturday'. Source: AAP

Kiongozi wa chama cha Labor Bill Shorten, anamwongezea waziri mkuu Malcolm Turnbull shinikizo ateme mipango yake ya makato ya kodi yamakampuni na ajiuzulu kutoka wadhifa wake wa waziri mkuu.


Hali hiyo imejiri baada ya chama cha Labor kupata ushindi mkubwa katika chaguzi ndogo za wikendi.

Matokeo ya chaguzi hizo ndogo, pia yame zua gumzo miongoni mwa mawaziri wa serikali ya mseto, kufanyia tathmini sera ya makato ya kodi hiyo.Nao maseneta huru Tim Storer na Derryn Hinch wamesema wako wazi kufanya mashauriano ila, bado watapinga mpango wa serikali ya mseto kufanya makato ya kodi ya makampuni makubwa.

Kwa sasa ni maseneta wanne huru kati ya maseneta huru kumi, ambao wame ahidi kuunga mkono muswada huo wa serikali.


Share