Dhamana ya nishati ya taifa inahitaji idhinishwa na serikali zamajimbo na mikoa pamoja na chama tawala, iwapo ita pata fursa yaku anza kutumika.
Kando na siasa za nishati, mmoja wa nyota wagombea wa chama cha Labor katika uchaguzi mkuu uliopita, ametangaza kuwa atajiuzulu baada ya wiki kibiliana na wiki kadhaa za kashfa dhidi yake. Hata hivyo Emma Husar, alifanya hivyo yeye mwenyewe masaa machache baada ya Bw Shorten kutoa kauli hiyo.
Bi Emma ametangaza hata tetea kiti chake cha ubunge katika uchaguzi mkuu ujao, ambao unatarajiwa kuwa mwaka ujao wa 2019, kwa sababu shinikizo imekuwa kubwa dhidi ya familia yake.
Licha ya madai yaliyo mkabili, imebainika katika uchunguzi ulio fanywa kuwa Bi Emma hana hatia yoyote.
Vikao vya bunge vita enza tena tarehe 13 Agosti, baada ya mapumziko marefu ya majira ya baridi.