Canberra: Tathmini ya wiki hii 30 Novemba 2018

Wabunge huru Kerryn Phelps (kushoto), na Julia Banks (kulia) ndani ya bunge la taifa mjini Canberra

Wabunge huru Kerryn Phelps (kushoto), na Julia Banks (kulia) ndani ya bunge la taifa mjini Canberra Source: AAP

Siku nne zina salia kwa vikao vya bunge mjini Canberra mwaka huu, serikali ya Morrison inajaribu kukwepa changamoto zaku aibisha kwa mamlaka yake bungeni.


Imekuwa wiki ngumu kwa serikali ya mseto, baada yakumpoteza mmoja wa wabunge wake wa kike ambaye ame amua kuwa mbunge huru, pamoja na tisho za wabunge wengine kufuata nyayo zake pia.

Vurugu ya wiki hii mjini Canberra ili sababisha mweka hazina wa taifa Josh Frydenberg, kufuta mipango yakwenda na waziri mkuu katika kongamano la G20 nchini Argentina.

Scott Morrison atakuwa katika mkutano huo wikendi hii pamoja na washiriki wake, kabla yakurejea nyumbani kushiriki katika vikao vinne vya mwisho wa mwaka.

 


Share