Canberra: tathmini ya wiki hii 7 Disemba 2018

Bill Shorten, (kushoto), na Scott Morrison (kulia) waenda kupiga kura ndani ya bunge

Source: AAP

Tamati ya kikao cha mwisho cha mwaka bungeni, ilikuwa yaku gadhabisha kwa wabunge na watazamaji wengi, baada ya hatua kadhaa zaku chelewesha sheria zaku fichua ujumbe wa siri, hatimae sheria hiyo ilipitishwa bungeni.


Hata kama serikali ilifanikiwa kupata ushindi katika dakika za mwisho kabla ya bunge kufungwa, si kila mtu aliye ridhika na jinsi wiki hii ilivyo kamilika katika bunge la taifa.

Kuna vikao sita tu vya bunge ambavyo vimeratibiwa katika mwaka wa 2019, kabla ya uchaguzi mkuu ambao unatarajiwa kufanywa mwezi Mei.

Iwapo mwaka huu ulikuwa mfano wa yatakayo jiri, bila shaka Canberra itakabiliwa kwa kimbunga chakisiasa katika mwaka wa 2019.


Share