Je kwa nini wahamiaji, hawataki kuhamia katika maeneo ya kanda ya Australia?

Duka lililo fungwa katika mji wa Broken Hill, magharibi ya NSW

Duka lililo fungwa katika mji wa Broken Hill, magharibi ya NSW Source: AAP

Takwimu kutoka idara ya maswala ya ndani zinaonesha kuwa, ni mhamiaji mmoja tu kati ya wahamiaji wanane nchini Australia ambao wana ishi nje ya miji ya Sydney na Melbourne.


Wakati kuna ongezeko la uhaba wa ujuzi katika maeneo ya vijijini na kandani, utafiti mpya kutoka Queensland umejaribu kuamua sababu kuu, zinazo fanya wahamiaji wasalie katika miji hiyo miwili mikubwa.

Mapema mwaka huu, serikali ya shirikisho ilipendekeza kuelekeza asilimia arobaini na tano ya viza za wahamiaji wakudumu, kuishi katika maeneo ya kanda au majimbo madogo kama Kusini Australia kwa miaka kadhaa.

Mpango huo ulizua maswali kuhusu jinsi serikali inaweza walazimisha wahamiaji kuishi kandani, bila kuingia katika mivutano yakisheria kuhusu kuzuia uwezo wa watu kusafiri.


Share