Elewa sheria za chanjo za watoto nchini Australia

a_child_receives_an_injection_during_the_vaccination_campaign_against_measles_rubella_and_polio_in_uganda_getty_0.jpg

Kuhakikisha mtoto wako anachanjwa humlinda, na inafaida kwa kila mtu wa karibu yake, wataalam wamesema.


Mahitaji ya chanjo kwa watoto hu tofautiana kutoka nchi moja kwa nyingine. Nchini Australia, sera za shirikisho za ‘No Jab, No Pay’ bila chanjo hukuna malipo na sera za jimbo za ‘No Jab, No Play’ ‘bila chanjo, hakuna kucheza’ zina hitaji watoto wapate chanjo kamili kulingana na mradi wa chanjo wakitaifa, kustahiki kupata malipo ya msaada wa familia au kupata huduma ya malezi ya watoto.

Wakati sera za chanjo za watoto hutofautiana, mantiki ya matibabu ina endelea kuwa thabiti duniani kote: miradi ya chanjo ime undwa kuwalinda watoto dhidi ya madhara mabaya ya magonjwa yaku ambukizwa.

Ime kadiriwa kuwa bila chanjo, mtoto mmoja kati ya watoto watano wanaweza kufa wakati wa miaka yao ya utotoni kwa sababu ya ugonjwa ambao hauko tena ndani ya jumuiya.

Jisajili au fuata makala yaliyo rekodiwa ya Australia yafafanuliwa kwa taarifa muhimu na, vidokezo kuhusu kuanza maisha yako mapya nchini Australia.

Je una swali lolote kuhusu au pendekezo ya mada? tutumie barua pepe kwa [email protected]

Share