Australia ilipokea idadi ya chini ya wahamiaji elfu ishirini kuliko mwaka ulio pita wa biashara, na viza takriban elfu kumi na mbili hazikutolewa na pia idadi ya viza ambazo hutolewa kwa uhamiaji wa familia nazo pia zilipungua kwa idadi ya elfu nane.
Peter Dutton ndiye waziri wa maswala ya nyumbani wa Australia, amesema kupungua kwa idadi hiyo ya wahamiaji imejiri kwa upande mmoja kama sehemu ya serikali kusikiza maoni ya jamii ila, wahamiaji na kundi za biashara zime sema kupunguzwa kwa mapokezi ya wahamiaji inaweza kuwa na matokeo mabaya.
Hatakama idadi ya wahamiaji wakudumu bado iko chini, kinacho julikana kama uhamiaji wakutoka ng'ambo kwa ujumla ni karibu 226,000 ya watu kila mwaka.
Uhamiaji wa ujumla kutoka ng'ambo unajumuisha watu wenye viza za muda mfupi pamoja na wa Australia ambao wana enda ng'ambo au wanao rejea nchini Australia baada yaku nje ya nchi kwa muda mrefu.
Idara ya maswala ya nyumbani imekadiria kuwa idadi ya watu ambao ni chini ya 512,000 ambao wame wasili nchini Australia kufikia mwisho wa mwaka wa biashara wa 30Juni2018. Na wakati huo huo idadi ya watu 286,000 waliondoka nchini Australia katika mwaka huo wa biashara.