Halmashauri za jiji 81 zafuta sherehe za viapo vya uraia katika siku kuu ya Australia

Australia Day

Melbourne's inner-city Yarra Council has decided to drop references to Australia Day Source: AAP

Takriban halmashauri za jiji 80 kote nchini Australia, zime amua kubadili tarehe ya sherehe za kila mwaka za viapo vya uraia kutoka Januari 26.


Wakati watu wengi wame pongeza uamuzi huo kama hatua katika mwelekeo sahihi, baadhi yawa Australia hawana uhakika kuhsusu uamuzi huo.

Zaidi ya miezi mitatu baada ya Australia kupiga kura yaku kana uwepo wa sauti yawa Australia wa Kwanza Bungeni, baadhi ya halmashauri za jiji zime chukua sheria mikononi mwao, kwa kubadilisha tarehe ya sherehe za kila mwaka za viapo vya uraia.

Januari 26 ni siku kuu ya Australia na, katika tarehe hiyo ndipo halmashauri za jiji huandaa sherehe za viapo vya uraia.

Ila hiyo ni tarehe pia katika 1788 iliyo ashiria mwanzo wa ukoloni, wangereza walipo peperusha bendera ya Uingereza katika bandari ya Sydney, nakudai ardhi hiyo kuwa koloni ya Uingereza.

Share