Katika jimbo la Magharibi Australia, Jamii ya Kitwek alikabiliwa na changamoto yaku endeleza tamaduni zao hususan kwa swala la tohara ya wavulana.
Licha ya nia yakushiriki kuwepo kutoka kwa wahusika, uwezo wakusafiri hadi nchini Kenya haukuwepo kwa sababu yakufungwa kwa mipaka yakimataifa ya Australia kwa sababu ya UVIKO-19. Hali hiyo iliwalazimisha viongozi wa jamii ya Kitwek kutafuta mbinu mbadala yakuwatendea vijana wao haki.
Katika mazungumzo maalum na Idhaa ya Kiswahili ya SBS Rais wa jamii ya Kitwek Bw Steven Sitienei, alifunguka kuhusu jinsi kamati yake ya viongozi ilivyo tatua changamoto hiyo. Bonyeza hapo juu kwa taarifa kamili.