Je! ushawahi kosa kazi "kwasababu ya kiwango chako cha Kiingereza" Australia?

Dr Kaitila (kushoto) kiongozi wa jamii yawa Tanzania na Bw Mike (kulia) kiongozi wa jamii yawatu kutoka DR Congo jimboni Queensland.

Dr Kaitila (kushoto) kiongozi wa jamii yawa Tanzania na Bw Mike (kulia) kiongozi wa jamii yawatu kutoka DR Congo jimboni Queensland. Source: SBS Swahili

Idadi ya watu wenye asili ya Afrika Mashariki na Kati, inaendelea kuongezeka kila mwaka jimboni Queensland.


Baadhi ya wanachama wa jamii hizo, wame dokeza kuwa moja ya kivutio cha kuishi Queensland ni sababu ya mazingira ambayo sitofauti sana na wanako toka.

Hata hivyo, maisha jimboni humo yana changamoto zake sawa na katika majimbo mengine ya Australia. Moja ya kero kubwa ikiwa ni ugumu ambao watu kutoka jamii za Afrika Mashariki na Kati hupitia, haswa wanapo tafuta ajira baadhi yao wakiombwa kuthibitisha ustadi wakiingereza licha ya wengi wao kufanyia elimu yao hapa nchini Australia.

Viongozi wa jamii yawa Tanzania Dr Sababu Kaitila na Bw Mike Fideli wa DR Congo, walieleza SBS Swahili baadhi ya hatua ambazo wamechukua, kuwatafutia wanachama wao afueni kwa kero hiyo pamoja na changamoto zingine wanazo kabiliana nazo. Bonyeza hapo juu kwa mahojiano kamili.


Share