Ila kabla uwe raia, lazima upite "Mtihani wa Uraia wa Australia". Mtihani huo hupima uelewa wako wa historia, tamaduni, maadili na mfumo wakisiasa wa Australia.
Katika makala haya ya Australia ya fafanuliwa, tuta kupa vidokezo pamoja na ushauri wakitaalam ambao utakusaidia kujiandaa kufanya mtihani wa uraia wa Australia.
Australia ni taifa lenye tamaduni mbalimbali, ambako zaidi ya vizazi 270 vinawakilishwa. Ni nchi ambayo ina fahari yakuwa na moja ya tamaduni kongwe zaidi inayo endelea, na imekaribisha takriban wahamiaji milioni saba tangu 1945.
Kuna njia kadhaa zaku wasilisha ombi la uraia wa Australia. Unastahili timiza vigezo maalum kabla yakuwasilisha ombi lako. 'conferral' na 'descent' ni moja ya njia za kawaida zaku omba uraia.