Jinsi yakujiunga na SES Australia

Maafisa wakujitolea wa SES, katika harakati za uokoaji Camden, Kusini Magharibi Sydney.

Maafisa wakujitolea wa SES, katika harakati za uokoaji Camden, Kusini Magharibi Sydney. Source: AAP Image/Dean Lewins

Panapo kuwa dharura inayo husiana na mafuriko, dhoruba na matukio mengine ya asili, watu wakujitolea huwa na sehemu mhimu kutoa jibu kote nchini Australia.


Ila je! Watu wanawezaje jiunga na huduma ya dharura ya jimbo au wilaya? Watu wakujitolea wanatarajiwa fanya nini na ni ujuzi upi wanahitaji kuwa nao kabla yakujiunga?

Huduma ya Dharura ya Jimbo inayo julikana kwa kiingereza kama The State Emergency Service (SES), ndilo jina ambalo hutumiwa na mashirika kadhaa nchini Australia, ambayo hutoa msaada wakati na baada ya matukio makubwa.

Shirika hilo hukabiliana na matukio ya asili kama mafuriko, dhoruba na tsunami ila, shirika hilo linaweza saidia pia katika dharura zingine kama uokoaji wima, uokoaji wa ajali za barabarani, utafutaji wa watu walio potea pamoja na uhamishaji wa matibabu. Kila mamlaka nchini Australia ina huduma yake ya dharura ya jimbo au wilaya.


Share